Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango yaridhia mpango wa kuanzisha ujenzi wa Shule ya mchepuo wa Kiingereza kwa kutenga shilingi Milioni 300 za Mapato ya ndani katika Bajeti ya mwaka 2024/2025 Wilayani Misungwi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya wakati wa kikao cha kupitisha rasimu ya mpango na Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Mapato ya ndani, ruzuku ya Serikali na Wafadhili kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 ambapo Kamati ya Fedha imeridhia na kukubali mpango ulioandaliwa na Menejimenti wa kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya mchepuo wa Kiingereza kwa ajili ya watoto wa madarasa ya awali na msingi itakayogharimu fedha shilingi Milioni 300 za mapato ya ndani kwa lengo la kuboresha elimu kwa Wananchi wa Misungwi kwa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora.
Awali akiwasilisha rasimu ya Bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Afisa Mipango Wilaya ya Misungwi Bi. Peniel Titus amesema kuwa Halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 51.4 kwa ajili ya utekelezaji wa wa shughuli mbalimbali za Halmashauri ikiwa ni pamoja na malipo ya Mishahara ya Watumishi kiasi cha shilingi Bilioni 36,792,448,000, fedha za Ruzuku ya uendeshaji wa Ofisi (OC) kiasi cha shilingi 1,359,841,000, pia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa shilingi Bilioni 8,636,386,000.
Bi. Peniel Titus amefafanua kwamba Halmashauri ya Misungwi imekisia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 4,677,820,361 kutoka vyanzo vya mapato ya ndani ambapo kati ya fedha hizo Bilioni 3,946,152,361 ni Mapato halisi na Shilingi Milioni 31,668,000 ni Mapato Lindwa na kwamba Mapato ya ndani kwa Mwaka 2024/202425 yameongezeka kwa asilimia 4.15 kutoka Shilingi Bilioni 4,483,664,000.04 mwaka 2023/24 hadi shilingi Bilioni 4,677,820,361.3 kutokana na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa matumizi ya mfumo wa kielektoniki wa ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa zinawekwa Benki kwa wakati, kuongezeka kwa watumiaji wa madini ujenzi hususani mchanga na mawe iliyopelekea kuongezeka kwa mapato ya madini ujenzi pamoja na kuongezeka kwa idadi ya viwanda na makampuni kupanda kwa ushuru wa Halmashauri.
Diwani wa Kata ya Misasi Mhe, Daniel Busalu akichangia hoja kuhusu kuanzisha ujenzi wa Shule ya watoto ya awali na msingi kwa mapato ya Ndani Bajeti ya mwaka 2024/2025 na wengine kulia ni abaadhi ya Madiwani wajumbe wa Kamati ya Fedha.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri wakisikiliza wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha kupitisha Bajeti ya mwaka 2024/2025
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.