Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza yashauriwa kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya uchimbaji wa Madini ujenzi ili kuwezesha na kurahisisha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini ujenzi ya kokoto na mchanga
Wito na ushauri huo umetolewa na Afisa Madini Mkoa wa Mwanza Nyaisari Mgaya Agost, 22, 2023 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha wanaweka maeneo maalumu yatakayotumika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ujenzi ili kuepusha uchimbaji holela ambapo hiyo itasaidia Halmashauri kuweza kukusanya mapato.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya amewaagiza watumishi wa Halmashauri kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea ya ukusanyaji.
Kwa upande Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Josefu Mafuru amesema kuwa wameweza kuimarisha ushiririkiano wa pamoja baina ya ofisi ya Tume ya madini Mkoa wa Mwanza pamoja na Halmashauri ili kujua idadi ya wachimbaji wadogo na kiasi cha madini yaliyokusanywa.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Mhe, Adelina Mathias ameiomba Ofisi ya Mkurugenzi ipange na kuweka utaratibu wa wachimbaji wote wenye leseni kuanza kutoa fedha za CSR zitakazosaidia kuleta mchango wa maendeleo katika Halmshauri ya Wilaya ya Misungwi.
Afisa Madini Mkoa wa Mwanza Bw,Nyaisari Mgaya aliyesimama akizungumza na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika ziara hiyo Ilifanyika katika Ofisi ya Tume ya Madini Ilemela Agosti,22,2023.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.