Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango yaridhishwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa vizuri na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe, Kashinje Machibya amepongeza Menejimenti na Watendaji kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali, Wafadhili na michango ya Wananchi.
Mhe. Machibya amesema kwamba kiujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana ambapo katika ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mabuki kupitia chanzo cha fedha cha BOOST kilichogharimu kiasi cha shilingi Milioni 351,500,000 mradi huo unaakwenda vizuri na upo katika hatua za utekelezaji .
Aidha Mhe, Machibya amewataka Wahandisi na Wasimamizi wanaosimamia ujenzi wa Miradi hiyo kuzingatia vigezo na ushauri uliotolewa na siyo vinginevyo, Sambamba na hilo amesema sehemu zinazohitaji marekibisho zifanyike kwa wakati kuondoa gharama zisizo za lazima.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama amesema kwa kushirikiana na Menejimenti ataendelea kusimamia kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha miradi ya maendeleo yote inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma bora inayostahili kwa wakati kwa kutumia ubunifu mkubwa wakati wa utekelezaji wa miradi husika na kwa kufuata miongozo na taratibu zinazotakiwa pamoja kuwa na ushirikiano na Watendaji, Viongozi na Wananchi wa maeneo husika kitendo ambacho kinaleta imani na kuongeza nguvu ya umiliki wa miradi hiyo kwa Wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi. Peniel Titus amesema kuwa ziara hiyo imelenga katika kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo miradi ilioyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Mabuki kupitia chanzo cha fedha cha BOOST kilichogharimu kiasi cha shilingi Milioni 351,500,000/= ujenzi wa shule ya Amali katika Kijiji cha Mhungwe chanzo cha fedha kutoka Serikali Kuu SEQUIP iliyotengewa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.