Kamati ya Afya ya Msingi yatakiwa kuhamasisha Wananchi na jamii kushiriki katika zoezi la Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Veronika Kessy mapema leo wakati akizungumza katika mafunzo ya Wajumbe wa Kamati ya Afya ya msingi ngazi ya Wilaya katika Ukumbi wa Mikutano wa Halamshauri
Mhe,Veronica Kessy amesema na kuwasihi wajumbe wa Kamati ya Afya ya jamii kwamba wanapaswa kutoa elimu na hamasa kwa jamii kuhusu zoezi hilo la Kampeni ya Chanjo ya polio na hivyo waweze kuondoa upotoshaji wa unaojitokeza kwa Wananachi kushiriki katika chanjo ya Polio ambayo inatarajiwa kutolewa mapema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Bw Benson Mihayo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya zoezi la Chanjo ya Polio na kuwataka Wajumbe wa kamati ya Afya y msingi kuanza kutoa elimu kwa Wananchi ili wajue faida na hasara za chanjo ya Polio itakayotolewa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano pamoja na kutoa matangazo ya hamasa na jamii iwe tayri kushiriki zoezi la Chanjo.
Naye Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma Wilaya Pauulina Lubimbi amesema kwamba katika Kampeni ya chanjo ya Polio awamu ya kwanza Wilaya ya Misugwi ilifanikiwa kwa asilimia 109 kwa kutoa chanjo kwa watoto wapatao 121, 101 na Kamati imejiandaa kufanya maandalizi ya hamasa kwa Wananchi kwa kushikisha wahamasishaji ngazi ya jamii ambao ni 295 watakaoweza kupita katika Kaya na kuwaeleza Wananchi kuhusu zoezi la Chanjo ya Polio.
Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma Bi, Paulina Lubimbi akijibu maswali ya wajumbe katika mkutano katika ukumbi wa Halmashauri ya Misungwi katika zoezi la kampeni ya Chanjo ya matone ya Polio .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Benson Mihayo aikihitimisha Mafunzo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri katika mafunzo ya zoezi la Kampeni ya Chanjo.ya matone ya Polio.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.