Jeshi la Jadi la Sungusungu latakiwa kuendelea kuweka ulinzi na Amani kwa kushirikiana na wananchi kuhamasisha maendeleo ya Taifa na uchumi imara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa na Balozi Mstaafu Mhe.Rajabu Omari Luhwavi jana alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Sungusungu kwa Kanda ya Ziwa uliokutanisha Mikoa minne ya Simiyu,Shinyanga,Mwanza na Tabora nakufanyika Kata ya Misasi Wilayani Misungwi.
Balozi Luhwavi ambaye ni mshauri wa Rais katika masuala ya Siasa na Uhusiano wa Jamii amesema kwamba Jeshi la Jadi la Sungusungu lina wajibu wa kudumisha ulinzi na amani wakati wa kutekeleza majumu yao ya kazi kwa kulinda mali za raia pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali maeneo yote.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Johari Samizi amefafanua kueleza kwamba Jeshi la Sungusungu lina mchango mkubwa katika kuhamasisha miradi ya maendeleo kanda ya ziwa hususan Wilaya ya Misungwi na kutoa wito kwa jeshi hilo kutowanyanyasa wananchi kwa kuwatoza faini ambazo hazikubaliki pamoja na kutumia utaratibu unaofaa pindi wanapo waadhibu watuhimiwa.
Kamanda wa Jeshi la jadi sungusungu Kanda ya Ziwa Mtemi Shimbi Morgan amesema na kusisitza kwamba jeshi hilo litaendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Serikali katika kudumisha amani na ulinzi na utulivu katika maeneo mbalimbali hapa nchini katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Hata hivyo Kamanda Morgan ameagiza viongozi wa jeshi hilo la jadi kuhakikisha matawi yote yanakuwa na sungusungu kwa kufuata utaratibu na vijana wajulishwe miiko ya sungusungu na taarifa hiyo ipate kwa kila mkoa,pia kuwataka viongozi kufanya kazi kwa kushiriana kila mmoja kwa nafasi yake.
Naye Diwani wa Kata ya Misasi Mhe.Daniel Busalu ametoa pongezi na shukrani za Pekee kwa Rais wa awamu ya sita Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya,Elimu,Maji na Miundombinu ya barabara kwa wananchi wa Kata ya Misasi na Wilaya ya Misungwi kwa ujumla wake.
Makamanda wa sungusungu kutoka sehemu mbalimbali katika Mikoa minne ya Kanda ya Ziwa wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Viongozi ngazi Taifa ambapo mkutano huo ulifanyika jana Kata ya Misasi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.