Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Mkoani Mwanza yatarajia kukusanya Mapato ya Ushuru wa shilingi Millioni 600 kutokana na Pamba iliyolimwa katika vijiji vyote 113.
Akizungumza na Timu ya Waandishi wa Habari wakati wa ziara ya Mkurugenzi ya kutembelea maeneo ya Miradi,katika Kata ya Lubili,Mkurugenzi Eliurd Mwaiteleke alisema kwamba amefurahishwa na mwitikio wa wananchi wa Misungwiwa kulima zao la Pamba ambalo Serikali Wilayani humu ilihamasisha kila Kaya Kulima Pamba angalau kuanzia hekari 2 na zaidi.
Mkurugenzi Mwaiteleke alibainisha na kuweka bayana kwamba Wananchi wamelima Zao la Pamba ikiwa ni agenda ya Mkoa na Taifa kwa ujumla na wameweza kukopeshwa mbegu,Viuatilifu na zana za Kilimo ambazo watalipa mara baada ya kupata mavuno.
Picha hapo juu,Katikati ni Silla Ntamuti Afisa Kilimo na Ushirika akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya Zao la Pamba kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Eliurd Mwaiteleke (Mwenye Skafu)
Alieleza kwamba Halmashauri inatarajia kupata mapato ambayo ni ushuru wa Pamba zaidi ya shilingi Millioni 600 katika msimu wa mwaka 2018 kutokana na Wananchi wengi kulima Pamba ambayo imestawi katika maeneo vizuri na inaendelea vizuri licha ya kuonekana changamoto ya kuvamiwa na wadudu katika baadhi ya mashamba.
Kwa upande wake Afisa Kilimo na Ushirika,Silla Ntamuti alisema kwamba Wilaya ya Misungwi wamelima Hekari 38,971 ambapo wamehamasisha na kuitikia Wito na matarajio ya kuvuna zaidi ya tani 21,000 za Pamba na wataalam wameweza kukabilana na changamoto ya ya wadudu walioshambulia zao hilo ikiwa ni pamoja na mvua zilizonyesha.
Aliwapongeza Wakulima waliojitokeza kulima pamba msimu huu na kuwaomba watakapopata mavuno waweze kulipa fedha za pembejeo walizokopeshwa kwa ajili ya mbegu na Viuatilifu .
Akifafanua kuhusu athari na madhara yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha Afisa Kilimo na Ushirika alieleza kwamba ni kweli mvua imeleta athari lakini hazina madhara yanayosababisha pamba kuduma mashambani na kwa sasa mvua hizo zinaelekea kukoma.
Katika Ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji ameweza kukagua na kuona shughuli na miradi mbalimbali ikiwemo Ukaranbati wa miundombinu katika Zahanati,Shule za Msingi na Sekondari na miradi ya Sekta ya Kilimo,Mifugo na Mazingira pamoja na barabara na Miundombinu ya Maji.na kuwataka Watendaji na Viongozi wa ngazi ya Kitongoji ,Kijiji na Kata kujituma na kuwajibika kila mmoja na kuwaletea Wananchi maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.