Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi,Angelina Mabula ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha Idara ya Ardhi na Maliasili kuandaa mpango Kabambe na kupima Ardhi ya Viwanja Elfu Moja katika malengo ya mwaka 2017/2018 ikiwa ni kuvutia Uwekezaji na kukuza maendeleo ya kiuchumi Wilayani.
Akizungumza na Viongozi pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya hii wakati wa Ziara ya kikazi aliyoifanya Wilayani hapa Mhe,Angelina Mabula aliiaagiza Menejimenti kuwa na mpango Kabambe katika masuala ya Upimaji wa Viwanja na kuleza kuwa malengo ya Halmashauri ya kupima Viwanja 250 kwa mwaka 2017/2018 hayakidhi Vigezo na hayaendani na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano na kuagiza Upimaji ufanyike angalau kufikia Viwanja Elfu Moja ikiwa ni pamoja na upimaji wa Ardhi ya maeneo ya Taasisi za Umma yakiwemo Mashule na taasis zingine,
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.