Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yapongezwa kwa kuwezesha mradi wa Elimu jumuishi ulioleta tija kwa watu wenye mahitaji maalumu Wilaya ya Misungwi, mradi huu unatekelezwa kwa kuimarisha maisha ya Wananchi na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia elimu ya msingi na Sekondari..
Hayo yamebainishwa tarehe 20 Novemba, 2024 na Wakurugenzi na Mameneja wa Mashirika manne yanayotekeleza mradi wa Elimu jumuishi wakati wa kikao cha pamoja na Afisa Mipango na Uratibu Bi. Peniel Titus kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama ambapo imeelezwa kuwa mradi unaotekelezwa na Sense Intenational umetoa fursa kwa makundi mbalimbali, ikiwemo wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, kupata mafunzo na rasilimali zinazohitajika ili kuboresha maisha yao na kutunaamini kuwa uwezeshaji huu utaleta mabadiliko chanya katika jamii zetu na kusaidia kupunguza umaskini.
Bi. Peniel ameongeza pia Mradi huo utatoa mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha, na mbinu za kilimo bora, ambayo yatasaidia wananchi kujenga uwezo wa kujitegemean ambapo ushirikiano kati ya Serikali, wadau wa maendeleo, na jamii katika kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi.
Vile vile Mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi Bw. Gerald Tupda ameeleza lengo la ziara hiyo ni kufanya tathimini juu ya mradi huo ikiwa ni pamoja na kuangalia kipi kiongezwe , kipi kiboreshwe na hali halisi ya ubainishaji watoto wenye ulemavu na kutoa elimu Jumishi kwa wanajamii ili kuona hatua zipi zichukuliwa kuboresha mradi huo.
Naye Afisa Michezo Wilaya ya Misungwi Bw. Joseph Mambo kwa Niaba ya Afisa Elimu Msingi amesema Shirika la Sense Intenational wamekuwa ni wadau wakubwa ambapo Misungwi jumla shule 15 zimenufaika nao na ni matumaini makubwa kuhusu mradi huu, wakisema kuwa utawasaidia kuboresha maisha yao na kuleta maendeleo katika maeneo yao ambapo ni hatua muhimu katika kuleta maendeleo endelevu wilayani Misungwi na unatarajiwa kuwa mfano wa kuigwa katika maeneo mengine nchini.
Kwa upande wake Meneja wa program ya Shirika la Sense Intenational Bi. Isabella Do Uugt katika ziara yake ya kutembelea shule ya msingi Shilabela pamoja na shule ya msingi Mitindo ametoa pongezi kwa mapokezi mazuri na kujionea mengi kuhusu mradi na kua ahadi ya kushirikiana na wadau pamoja na Serikali .
Akitoa shukrani za pongezi Mwenyekiti wa Sauti ya Wanawake wenye ulemavu Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Agness Makambajeki amesema wanajukumu la kubainisha na kutoa elimu jumishi kwa wanajamii pamoja na kukutana na wazazi na kuwaelimisha kuwapeleka watoto wenye changamoto ya ulemavu shule.
Ziara hiyo ya kutembelea shule za msingi na miradi iliyotekelezwa imefanyika katika maeneo ya Shule ya Msingi Mirtindo na Shule ya msingi Shilabela ambapo mashirika manne ya Sense Intenational Tanzania, Add Intenational, Light for the World, na Tanzania Chashire Foundational yaliweza kuona shughuli zilizofanyika wakiambatana na baadhi ya Wawakilishi wa (OPD), Kamati za Watu Wenye ulemavu, pamoja na Wataalam wa Halmashauri wanaoshiriki kwenye mradi wa Elimu Jumuishi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.