Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yajipanga kikamilifu kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 utakaopokelewa katika Kijiji cha Mwasonge tarehe 10 Oktoba, mwaka 2024 Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza.
Hayo yabainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024, ameeleza kwamba Halmashauri ya Misungwi ipo tayari na imejipanga kikamilifu na kuhakikisha kwamba Mwenge wa Uhuru unapokelewa vizuri na kuhakikisha uwepo wa hamasa kubwa na Wananchi wanajitokeza kwa wingi ambapo tayari maandalizi yote yanaenda vizuri na kwa upande wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaendelea vizuri tayari kwa ajili ya kuzinduliwa, kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Mhe. Samizi ameongeza kuwa katika kuhamasisha maendeleo na uzalendo miongoni mwa Wananchi Hamasa ya kushiriki kikamilifu ni sehemu ya kudumisha hali ya umoja ambapo taratibu zote za mapokezi zinafanyika kwa kiwango cha juu ili kupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 katika mazingira bora na yenye shamrashamra.
Kwa upande wake Mratibu wa mbio za Mwenge wa Uhuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw. Sixbert Mbwambo ameeleza kuwa Wanakamati na wadau mbalimbali wamejipanga vizuri kwa ajili ya mapokezi ya Mwenge huo ambapo maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na suala la Hamasa kwa Wananchi ili kuhakikisha Wananchi wanashiriki kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa wingi na kuukimbiza kupitia katika miradi iliyopangwa ikiwa na kushiriki Mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa CCM Misasi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 zinakimbizwa zikiwa na Kauli mbiu ya “ Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu’’ na kwamba Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 zinatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri 8 za Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 6 oktoba hadi tarehe 13, pamoja na Sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru Kitaifa zitafanyika tarehe 14 oktoba mwaka 2024 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.