Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi yafanya ziara ya yatembelea na kupata mafunzo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya nyang'hwale kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika ukusanyaji wa mapato ya madini Mkoani Geita.
Akizungumza hii leo tarehe 25 Aprili 2025 wakati wa ziara hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw. Abdiel Makange amesema tumefika katika Halmashauri ya Wilaya ya nyang'hwale kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kwenye ukusanyaji wa mapato ya madini ili kuona namna gani tunazingatia upatikanaji na ukusanyaji wa mapato hayo ya madini
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri Wilaya ya Misungwi Mhe. Erasto Machibya amesema kuwa ziara hio sio tu kubadilishana uzoefu bali pia Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambao pia ni wajumbe wa kamati ya huduma ya jamii, wakuu wa idara na vitengo wamekagua shule ya private ya halmashauri ya nyang'hwale.
Naye Afisa utumishi Wilaya ya Misungwi Bi, Samina Gullam kwa niaba ya Menejimenti ya Utumishi wakiwemo Wakuu wa idara na vitengo amesema kuwa wamejifunza na kuona utendaji kazi ulivyo katika Halmashauri hio na kuwataka watendaji kuviishi vile ambavyo wamevipata kutoka halmashauri ya wilaya hio kwa ajili ya kubadilishana uzoefu huo walio upata katika ukusanyaji wa mapato ya madini.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.