Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ametoa wito kwa watumishi na watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na kujituma katika kufanya kazi ili kupata matokeo chanya wakati wa kutekeleza Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa leo, na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi katika Kata tatu ikiwemo Kata ya Shilalo,Buhingo na Kata ya Gulumungu ambapo alikagua miradi mbalimbali na kuongea na Walimu wa Shule ya Sekondari Shilalo ili kujua changamoto zinazo wakabili watumishi hao, na kuridhishwa na maendeleo ya shule hiyo.
Bw.Mafuru ameagiza shule zingine za Sekondari za Halmashauri kwenda kujifunza katika shule hiyo na kuiga mfano mzuri kwani imefanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa kushika nafasi ya kwanza kiwilaya mara tatu mfululizo sambamba na kutoa chakula cha kutosha shuleni hapo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji ametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Zahanati ya Nyashitanda,vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi nyashitanda na matundu manne ya vyoo katika shule ya Kisesa ambapo ametoa maelekezo kwa mtendaji wa Kata kufikia tarehe 1,Julai 2024 matundu ya vyoo hivyo yawe yamekamilika na taarifa aipate ofisini kwake.
Katika hatua nyingine Bw.Mafuru ametembele na kujionea hatua ya ujenzi wa mradi wa Zahanati ya Seke,ujenzi wa shimo la choo katika gulio la mnada wa Seke uliopo Kata ya Buhingo pamoja ujenzi wa vyumba viwili katika shule ya Mwakiteleja,ujenzi korido katika Zahanati ya Nyamainza na ujenzi wa nyumba la daktari katika Kata ya Gulumungu ambapo ameahidi kupeleka fedha kwa wakati kwa miradi ambayo haijakamilika.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Shilalo Mhe.Mayila Maguha ametoa shukrani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo hususan mradi wa Zahanati ya Nyashitanda kwa wananchi wa Shilalo.
Naye Diwani wa Kata ya Buhingo Mhe.Marco Kadala amesema kuwa ujenzi wa Zahanati ya Seke upo katika hali ukamilishaji ambapo mpaka sasa umetumia fedha shilingi milioni 28 na kuwashukuru wananchi kwa kushiri katika ujenzi wa zahanati hiyo na kuiomba Serikali iongeze nguvu katika kukamilisha ujenzi, na huduma ianze kutolewa kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru wa pili upande wa kulia, akiongea na Walimu wa Shule ya Sekondari Shilalo leo mapema wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi,ambapo ameridhishwa na maendeleo ya shule hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru akisikiliza na kupokea taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Nyashitanda kutoka Diwani wa Kata ya Shilalo Mhe.Mayila Maguha leo mapema katika ziara ya kukagua miradi ambapo ameridhishwa na ujenzi wa zahanati hiyo.
Muonekano wa jengo la Zahanati ya Nyashitanda ambapo mpaka sasa iko katika hali ya ukamilishaji,pindi itakapokamilika itasaidia kuondoa adha ya umbali mrefu kwa wananchi wa Kata ka Shilalo kwenda kutafuta huduma za afya.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.