Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi awataka watumishi wa umma kuacha tabia ya kutoa na kupokea rushwa katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa tarehe 24, Februari,2024 na Mkuregenzi wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Kata ya Mbarika Wilaya ya Misungwi.
Bw. Mafuru ameeleza na amefafanua kwamba kumekuwa na wimbi la watumishi kupokea rushwa kipindi wanapotoa huduma za afya katika Vituo vya Afya na Zahanati na kutoa onyo kali kwa mtumishi yeyote wa umma atakaye jihusisha na kitendo cha kutoa na kupokea rushwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo na hasa katika Sekta ya Afya.
“Kuna kashfa ya rushwa sana gari la wagonjwa Serikali imetoa bure mafuta ni ya Serikali hivyo toeni huduma bure, sehemu ninayoingalia kwa tahadhari ni kwenye eneo la Afya”Alisisitiza Mkurugenzi Bw.Mafuru.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi.Samina Gullums amewa kumbusha watumishi wa Halmashauri hiyo kuwa na nidhamu katika utendaji kazi,kuzingatia mavazi yenye heshima wanapokuwa kazini na baada ya kazi na kuzingatia lugha nzuri wakati wote wanapo hudumia wananchi.
Sambamba na hayo Bi.Gullums ametoa rai kwa watumishi wote Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuendelea kujifunza kwa bidii mfumo wa PEPMIS ambapo zoezi la kuingiza majukumu katika mfumo limeisha na zoezi linaloendelea sasa ni kuingiza kazi za kila siku na endapo mtumishi hataingiza kazi zake kwenye mfumo huo ambao umeunganishwa na mfumo wa mishahara atakosa stahiki zake kupata mshahara.
Naye, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Christopher Legonda ametoa wito kwa Viongozi na Watendaji kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa Wananchi na Wazazi kuendelea kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi waweze kupata mlo kamili wawopo shuleni.
Bw.Legonda amefafanua kwamba Serikali inatoa fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo na kuwataka watenda wa kata,Vijiji na Walimu kusimamia kwa kikamilifu na kuwashirikisha wananchi katika miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kuacha vitendo vya udokozi ambavyo vinaweza kuleta migogoro kwa wananchi.
Wakati huo huo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Clement Morabu ameeleza na kusistiza kwamba watumishi hasa Sekta ya Afya watoe huduma nzuri kwa wananchi na kutumia lugha zenye staha wanapo wahudumia bila kubagua mtu yeyote na kuongeza kuwa gari la wangojwa ambalo lilikuwa limeharibika ndani ya wiki mbili litakuwa limetengemaa na kuhudumia watu wa tarafa ya Mbarika.
Baadhi watumishi wa Tarafa ya Mbarika wakifuatilia na kusikiliza maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji katika kikao hicho ambacho kilichofanyika siku ya Jumamosi katika shule ya sekondari Mbarika.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi. Samina Gullums akiongea na Watumishi wa Tarafa ya Mbarika ambapo aliwataka kuzingatia maelekezo waliyoyapewa katika kikao hicho.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.