Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza watakiwa kufanya kazi kwa Weledi na Unyenyekevu na kutimiza ndoto katika maisha yao.
Wito huo umetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Benson Mihayo wakati akaizungumza katika kikao cha Watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa Halamshauri hiyo.
Bw. Benson Mihayo alieleza kwamba katika utumishi wa umma ni vyema kila mmoja akatimiza wajibu wake na Watumishi wote wanapaswa kufanya kazi kwa kupendana na kusaidiana ambapo Watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa undugu na kushauriana katika mambo na sekta zote zikiwemo utekelezaji wa miradi pamoja na ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.
“Binadamu aliyezoea kula nyama ya binadamu hawezi kuacha “ Alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Katika kikao hicho Bw,Benson aliwataka Watumishi wote wasaidiane na kushauriana katika kutekeleza majukumu kwa kushirikiana kwa lengo la kufanya kazi kwa uzalendo na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mihayo alisisitiza Watumishi wote kufanya kazi kwa Unyenyekevu na watiifu katika kazi hivyo waondoe kiburi,kwa kufanya hivyo itwasaidia kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kujiamini kwa kutanguliza maslahi ya watu wengine na kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.Sambamba na hilo alisisitiza Watumishi kujituma katika kazi na kuwa wazalendo.
Amewasihi Watumishi wajitahidi na kuongeza bidii katika utafutaji wa maisha mazuri katika Nyanja tofauti tofauti na sekta mbalimbali na kuacha tabia ya ubinafsi na kukumbatia mambo ambayo haya tija katika maisha yao na badala yake kufanya kazi kwa bidii na kutumisha ndoto za wengine.
“Nawambia ndugu zangu tusiue ndoto za Watumishi,sisi ni familia moja lazima tuwe na mshikamano na Upendo kwa kufanya hivyo tunatembea kwa pamoja na tutaweza kuendeleze ndoto za wenzetu”.Alisema Benson Mihayo.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Utumishi Said Ally alisema Watumishi wanatakiwa kufika kazini kwa muda uliopangwa na si vinginevyo na kufuata taratibu,kanuni na sheria za utumishi wa umma katika kutekeleza majukumun yao ya kazi ya kila siku.Sambamba na hilo wametaka watumishi kuzingatia utoaji wa taarifa uzingatie itifaki na si kutoa kiholela ili kutoleta taharuki yeyete ambayo inaweza kujitokeza na kuleta usumbufu kwa Watumishi.
Hata hivyo Bw,Ally alihimiza Watumishi wa Halmashauri ya Misungwi kuzingatia suala la usafi wa mazingira kwa ujumla kwa kuweka mazingira katika hali ya usafi maeneo ya ofisi na vyooni na kutunza vifaa na samani za ofisi,na kuwakumbusha wanahakikishe takataka zote zihifadhiwe sehemu sahihi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Bw,Benson Mihayo akizungumuza na Watumishi katika ukumbi wa Halmashauri katika kikao kazi mapema leo,kulia ni Kaimu Afisa Utumishi Said Ally.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, kushoto ni Afisa Elimu Sekondari Bi, Diana Kuboja,anayefuata ni Mkaguzi wa ndani Bw, Sindaguru Jonas na kulia ni mtunza Hazina Bw, Joseph Mazito wakisikiliza kwa makini na kupokea maelekezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi katika kikao kazi mapema leo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.