Mkuu wa Wilaya ya Misungwi awataka Wachimbaji wa dogo kuwa na umiliki wa leseni ya uchimbaji madini ili kujikwamua kiuchumi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Johari Samizi ameyasema hayo leo tarehe 05,Juni,2024 wakati wa kusikiliza na kutatua kero kwa wananchi wa Kijiji cha Mwanangwa Kata ya Mabuki ambapo amewataka wachimbaji hao wadogo kuwa na leseni za kuchimba madini na kufuata utaratibu pindi wanapoanza shughuli za uchimbaji wa madini ili kuondokana na migogoro isiyokuwa yalazima.
Mhe.Johari Samizi emeeleza na kufafanua kuwa Serikali inafanya kila namna kuhakikisha ina mnyanyua mwananchi wake kiuchumi na kwamba Serikali ina watambua wachimbaji wadogo hivyo imeweka mazingira rafiki kwa wachimbaji hao kwa kusogezwa karibu masoko ya kuuzia madini ili kuepuka kutepeliwa na watu wasiokuwa na nia njema.
Aidha Bi.Samizi amesema kuwa Wananchi wanalo jukumu la kuwalinda na kuwatunza watoto wa kike na wa kiume,kupinga ukatili dhidi yao,kutowapa mimba wanafunzi na kuhakikisha wanapelekwa shule kupata elimu kwani ni haki yao ya msingi, sambamba na hilo amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti na hasa miti ya matunda ili kuendana mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wake Mhandisi Mwandamizi wa madini Mkoa wa Mwanza Bw.Ndembi Tuma emetoa wito kwa wachimbaji wadogo kufuata taratibu za kisheria za kumiliki leseni za kuchimba madini na kuzihuisha leseni zao pindi zinapoisha muda wake na kuwataka wafike kwenye ofisi za madini kulipia leseni hizo.
Naye diwani wa Kata ya Mabuki Mhe.Malele Lutoja ameishukuru Serikali kwa kupeleka fedha nyingi zaidi Bilioni 1 katika kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Afya,Elimu,Umeme na barabara kwa wananchi wa Mabuki.
Diwani wa Kata ya Mabuki Mhe.Malele Lutoja akiongea na wananchi wa kijiji cha mwanangwa mapema leo,na kuwataka wananchi hao kuendelea kuunga juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Wananchi wa kijiji cha Mwanangwa Kata ya Mabuki wakisikiliza na kutoa changamoto na kero kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Johari Samizi leo mapema katika mkutano wa hadhara.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.