Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha aridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Boost wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1,512,500,000/= zimetumika katika mradi huo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza
Hayo yamebainishwa katika ziara Ukaguzi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Miradi Wilayani Misungwi Mhe, Paulo Chacha ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Boost ambapo miradi hiyo iliyokuwa na lengo la kutoa elimu bora kwa Wanafunzi kupitia ujenzi wa Madarasa yaliojengwa, vyoo pamoja na madawati uliotekelezwa kwa Shule za Msingi tisa Wilayani humo.
Mhe, Chacha amesema kupitia Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Misungwi imefanikiwa kupata fedha na kuhakikisha kazi hizo zinafanyika kwa kasi ambayo inaridhisha ambapo changamoto kama vile huduma ya maji na umeme zimewasilishwa na zimetatuliwa na zitaendelea kushughulikiwa kwa wakati kabla ya mwezi Disemba mwaka 2023 ili kurahisisha shughuli za kuongeza kiwango cha elimu Wilayani nataifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Mhe, Abdi Makange akiwa katika kijiji cha Mwakiligili Wilayani Misungwi amesema Watumishi wamejitaidi kikamilifu katika kuhakikisha miradi hiyo ya Boost Wilayani Misungwi umezidi kwenda vyema kwa kujengwa kwa kiwango cha hali ya juu na hatimaye kukidhi na kujibu changamoto za watoto kutokwenda shule kwa uhaba wa majengo ya madarasa pamoja na madawati.
Mhe, Makange amewasihi na kuwataka Wananchi na Wakazi wa Kijiji cha Mwagiligili kuyatunza na kuyalinda madarasa ,madawati pamoja na vyoo ili kuwanufaisha wao na kizazi kijacho na kuwakumbusha wazazi kuwahimiza na kuwapeleka watoto shule ili wapate elimu na maadili mazuri.
Naye Afisa Vifaa na Takwimu Msingi Wilaya ya Misungwi na Mratibu wa Mradi wa Boost na SWASH Bw Godfrey Majura amesema kiasi kilichotengwa kwa ajili ya mradi wa boost ni shilingi bilioni 1,512,500,000/= kwa shule takribani 9 zimefikiwa na mradi huo.
Bw Godfrey Majura amesema shule takribani 2 ambazo ni shule ya msingi Mbela na shule ya msingi Ntende (Mwabebea) zimejengwa upya na shule zilizobaki takribani 7 kufanyiwa ukarabati na nyongeza ya kujenga majengo ya Madarasa pamoja na vyoo hivyo zoezi la ujenzi limefanyika vizuri na kwa ubora.
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Shilalo Bw, Samson Selema amesema kuwa hapo awali watoto walikua wakipata adha kubwa wakiwa darasani kwani iliwabidi kujazana hatimaye hali hio kwa sasa imetatuliwa ambapo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Misungwi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo y sekta zote ikiwemo elimu na kuwaomba waendelee na moyo huo ili kuwletea maendeleo ya dhati Wananchi.
Halmashauri ya Misungwi imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya, Barabara, Maji pamoja na sektaya Elimu ambapo kwa upande wa elimu kupitia mradi wa Boost imeweza kutekelezashile hizo mi pamoja na shule ya msingi mbele,shule ya msingi kagera,shule ya msingi ntende ,shule ya msingi iteja,shule ya msingi nyabuhele,shule ya msingi chatta,busegeja shule ya msingi,igwta shule ya msingi,shule ya msingi mwagiligili.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha akikagua Mradi wa BOOST katika Shule ya Msingi Kagera Kata ya Usagara hivi karibuni ambapo aliridhishwa na Mradi huo.
Mwonekano wa baadhi ya Majengo ya Mradi wa BOOST yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 miongoni mwa Shule tisa katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.