Maafisa Ugani Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza waagizwa kuwatembelea Wakulima wa kilimo cha pamba mashambani na kutoa ushauri na maelekezo ya kulima kitaalamu ili kupata mazao ya kutosha katika msimu huu.
Akizungumza katika uzinduzi wa msimu wa Kilimo cha Pamba katika Kijiji cha Maganzo Kata ya Mondo Wilayani humu Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda amewaagiza Maafisa Kilimo wote kuhakikisha wanawatembelea Wakulima wa pamba na kuona hali na maendeleo ya kilimo na kutatua changamoto wanazokumbuna nazo kwenye kilimo na kuwashauri kulima kitaalamu.
Amewataka maafisa Ugani kuwafuata Wakulima mashambani na ktatua changamoto zote za Kilimo na kuwashauri na kupata takwimu na taarifa zote za Wakulima wanalima mazao gani na Hekari ngapi na maendeleo yote kwa ujumla.
“ Ni aibu sana unamkuta kijana anacheza bao na karata wakati huu wa Kilimo na kuagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kuwakamata wote wanaozurula na kucheza bao na kuhakikisha wote wanaenda kulima mashambani na kuzalisha” Amesisitiza Juma Sweda.
Juma Sweda amewataka Wananchi wote kuendelea kulima kilimo cha Pamba kwa lengo la kujipatia fedha na kujiongezea kipato na kuimarisha uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Amewasihi Wakulima pia kulima mazao ya Chakula likiwemo zao la Viazi vitamu na mahindi ili kuweza kuongeza upatikanaji wa Chakula na kujenga afya na maisha ya Wananchi, na na kueleza kwamba msimu umeanza kila mtu aanze kulima na kuacha uzembe na uvivu hivyo Waanchi wote wanapaswa kuwajibika katika Kilimo na kuzitumia vyema mvua za vuli.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kwilasa Mahigu ameeleza katika taarifa ya Idara kwamba Halmashauri katika msimu huu wa 2020/2021 wamepanga kulima mashamba ya pamba zaidi ya Hekta elfu kumi mia sita themanini na saba (10,687) ambapo wastani wa Wakulima wanaolima zao la Pamba ni asilimia 56 waliopo kwenye Kaya zipatazo elfu thelethini mia nne na kumi na nane (30,418) na wanatarjia mavuno ya Pamba yapatayo tani 10,687.
Amesema kwamba mikakati iliyowekwa ni pamoja na kuhamasisha Wakulima wengi kujitokeza kulima zao la pamba ili kupata mavuno bora na kuleta tija katika kilimo cha pamba Wilayani Misungwi pamoja na kuwa na mashamba ya mfano ambapo Maafisa Ugani wote wameelekezwa kuwa na mashamba ya mfano na kulima kwa mfano sambamba na hilo wanatakiwa kusimamia na kushauri wakulima wasiopungua kumi na tano.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda (wa pili kulia) akipanda mbegu za Pamba wakati wa Uzinduzi wa msimu wa Kilimo cha Pamba katika shamba la Mkulima mmoja Kijiji cha Maganzo Wilayani Misungwi, akiwa na baadhi ya Viongozi wa Wilaya akiwemo Katibu Tawala Petro Sabatto (wa kwanza kulia) pamoja na Wakulima walioshiriki zoezi la Kilimo cha Pamba.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.