Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Johari Samizi, amewataka Wazazi na Walezi kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa Watoto wao ili kulinda mila na desturi na kukuza maadili katika jamii kwa lengo la kuzuia vitendo viovu na kuimarisha maadili mema Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhe. Samizi ametoa wito huo wakati wa kikao cha Hadhara kilichofanyika tarehe hivi karibuni katika Kata ya Isenengeja kikiwa na ajenda kuu ya ulinzi na usalama amesema kuna umuhimu mkubwa kushirikiana katika ulinzi na usalama baina ya Wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuhakikisha amani na utulivu katika jamii aambapo suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mmoja, hivyo Wananchi washirikiane na Jeshi la Polisi na Viongozi wa mitaa pamoja na Sungusungu katika kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya kihalifu, Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo wizi wa Mifugo na uvunjifu wa amani, na kwamba hatua madhubuti zinaendelea kuchukuliwa kukabiliana na matatizo hayo.
Kwa upande wake Katibu wa Sungusungu Kata ya Isenengeja Bw. Sitta Machama wakati akisoma Risala kwa mgeni Rasmi ameleza kuwa changamoto zinazowakabili ni uhaba na ukosefu wa maeneo ya malisho kwa Wafugaji na Wakulima katika kipindi cha kilimo ambapo mara nyingi Wafugaji wanakosa maeneo ya kuchungia mifugo yao kwa sababu ya ufinyu wa mashamba vitendo hivyo vinasababisha kero na hasara kwa pande zote, huku wakulima wakikumbwa na uharibifu wa mazao kutokana na mifugo kuingia kwenye mashamba hayo.
Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Lwelwe Mpina kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa kazi ya vyombo vya usalama ili kupambana na uhalifu na kuimarisha amani lakini ni muhimu kushirikiana kati ya Wafugaji na Wakulima katika kutafuta suluhu za muda mrefu, ikiwemo kuanzisha maeneo ya malisho maalum na kuboresha matumizi ya ardhi ili kukabiliana na changamoto hizo, na kutoa wito kwa Wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kushughulikia masuala haya kwa ukamilifu.
Wilaya ya Misungwi inaendelea na kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 zinazotarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri 8 za Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 6 oktoba na kuhitimishwa oktoba 14 Jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “ Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu ”. ambapo baadhi ya maeneo ya Vikundi vya sanaa pamoja na Jeshi la Sungusungu wanajinoa kwa ajili ya hamasa ya sherehe za Mwenge na ushiriki wa Wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.