Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi awataka Wakulima kuzingatia kanuni bora za Kilimo cha Zao la Pamba ili kuongeza tija katika Uzalishaji Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika Viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi katika Hafla fupi ya makabidhiano ya Baiskeli tarehe 4 Novemba 2024, Mkuu wa Wilaya ya Msungwi Mhe. Johari Samizi amesema kuwa bodi ya Pamba imewaamini na kutoa Baskeli hizo kwa lengo la kuzitumia ili kuimarisha kilimo cha zao la pamba.
Mhe. Johari Samizi amesema na kuwaelekeza Wakulima hao kuvilinda na kuvitumia vizuri vyombo vya Usafiri wa Baiskeli kwa matumizi yaliyokusudiwa ili waweze kuwapa manufaa ya kiuchumi na kuinua kipato chao pamoja na kuhakikisha Wakulima wote wanapatiwa elimuna kuhamsishwa namana ya kulima Kilimo cha Pamba kwa kuzingatia kanuni 10 bora za Kilimo cha zao la Pamba kwa lengo la kuongeza tija nkatika uzalishaji wa Pamba nchini na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
“Mkatumie vyombo hivi kuwaelimisha Wakulima kwa kuzingatia kanuni kumi za upandaji na uvunaji wa zao la pamba , tukatumie vyombo hivi ili kupata tija , kipato cha kutosha kwa wakulima na Halmashauri itapata mapato ya ndani kupitia malighafi hiyo ” Alisisitiza Mhe. Johari Samizi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Bw. Addo Missama, amesema kuwa wakati wa makabidhiano hayo, ni muhimu kwa wakulima kuzingatia matumizi sahihi ya Baiseki hizo ili kupata matokeo bora ambapo halmashauri itaendelea kuimarisha njia bora za kuwanuifaisha Wakulima wa zao la pamba ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa hivyo ili kuhakikisha wakulima wanapata faida kubwa.
Akiwasilisha taarifa ya makabidhiano ya Baiseki hizo, Mkaguzi wa Pamba Wilaya ya Misungwi, Bw. Lazaro Mashauri amesema umuhimu wa vifaa hivyo kwa Wakulima hao kuboresha uzalishaji wa pamba katika eneo hilo ambapo Baiseki hizo zitasaidia wakulima kuongeza tija na ubora wa mazao yao, hivyo kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya jamii.
Naye, Diwani wa Kata ya Kijima Mhe. Ezekieli Kanzaga amesema kuwa makabidhiano hayo ni fursa pekee na hatua muhimu katika kusaidia Wakulima wa pamba katika Kata hiyo ambapo ushirikiano kati ya Serikali na Wakulima ni muhimu ili kufanikisha malengo ya kilimo endelevu cha zao la pamba.
Wakulima wawezeshaji kutoka Kata ya Kijima Bi. Leticia Gwancha na kata ya Idetemya Bw. Dominiko Elias wameeleza furaha yao na shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia baiskeli kupitia Bodi ya Pamba ambapo Baiskeli hizo zitawasaidia kuboresha usafiri wao wakati wa shughuli za kilimo, hivyo kuongeza uzalishaji na tija katika mazao yao ya pamb pia baiskeli hizo zitawasaidia kufikia masoko kwa urahisi zaidi, na hivyo kuongeza kipato chao na kuboresha maisha yao na familia zao.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.