Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amewapongeza Waalimu wa Shule za Sekondari kwa ufaulu wa Matokeo ya Kidato cha Nne 2024, kutoka 96.4% mpaka 99.75 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza mapema hii leo Tarehe 16 Mei 2025 katika Hafla ya kuwapongeza Waalimu na Kuwapa motisha Waalimu iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi CDTI ambapo Mhe.Samizi amesema kuwa pamoja na kupongeza kwa juhudi za ufaulu kwa Waalimu hao ni vyema pia tukashiriki Uchaguzi kwa kila Mwananchi aliye na sifa ashiriki katika kumchagua Rais, Mbunge na Diwani amtakaye.
Katika hatua nyibgine Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw. Abdi Makange amesema kuwa hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirikiano ambao ni fahari yetu kuendelea kuishi kwa amani.
Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Mhe. Kshinje Machibya ametoa pongezi kwa Waalimu Wilayani humo kuwa na ufaulu wa Wanafunzi wa Kidato cha Nne 2024 kwa juhudi za maendeleo ya jamii kama elimu ni sehemu ya kutoa na kuandaa wataalamu katika Taaluma mbalimbali kwa ajili ya Taifa la kesho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi amesema kuwa katika hafla hiyo Walimu ambao shule zao zimepata ufaulu wamepewa zawadi mbalimbali ikiwemo tukunukiwa cheti, Runinga(Tv) na nyenginezo ambazo zinalenga kutoa motisha na kuongeza chachu ya Mafanikio katika ufaulu kwa Wanafunzi.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Misungwi kwa niaba ya Waalimu Wilayani humo ametoapongeza kwa mapokezi na ufanikishaji wa hafla hiyo kwa Viongozi ngazi ya Mkoa, Wilaya hadi kata kwa kuwa sehemu ya kupata ufaulu wa matokeo ya kidato cha Nne kwa Mwaka 2024 kwa asilimia 99.75 ambapo Mwaka 2021 hadi 2024 kiasi cha Shilingi Bilioni 6,760,449,570.53 zimepokelewa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Shule mpya za Sekondari, Vyumba vya Madarasa kwa lengo la kupunguza mlundikano wa Wanafunzi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.