Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mkoani Mwanza,Mhe,Juma Sweda aiagiza Kamati ya Shule ya Msingi Isela kuhakikisha Wanafunzi wanahama kutoka Shule ya Msingi Busagara kwenda katika Shule ya Msingi mpya ya Isela mara baada ya kukamilika kwa vyumba vinne vya madarasa vya Shule hiyo.
Akizungumza wakati wa Ziara ya kikazi katika Kata ya Usagara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe,Juma Sweda aliutaka Uongozi na Kamati ya Shule ya Msingi Isela kuhakikisha inawahamisha Wanafunzi hao na kuanza kusomea katika vyumba vinne vya madarasa vya Shule hiyo vilivyojengwa na kukamilika mwezi Julai mwaka 2018 ili kuweza kusaidia watoto wa Shule kusoma vizuri na kuleta tija na hatimaye kuongeza ufaulu kutokana na mazingira bora ya kufundisha na kujifunzia.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe, Juma Sweda akikagua Ujenzi wa Vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Msingi Isela .
Mhe, Juma Sweda alishangazwa na kusikitishwa baada ya kukagua na kukuta vyumba hivyo vya madarasa kukamilika lakini Wanafunzi hawajaanza kuvitumia badala yake wanaendelea kubanana katika madarasa ya Shule ya Msingi Mama ya Busagara,amewataka Viongozi wa Halmashauri,Kamati ya Shule kutekeleza agizo hilo kufikia siku ya Jumatatu tarehe 1 oktoba 2018 tayari Wanafunzi waanze kusomea katika Madarasa hayo.
Amewataka Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Idetemya wakishirikiana na Kamati ya Shule kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa Shimo la Choo cha Wanafunzi ndani ya Wiki mbili kwa kutumia nguvu kazi na michango ya Wananchi kwa ajili ya matumizi ya Wanafunzi na kuondokana na milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Kichocho,Minyooo na UTI yanayosababishwa na ukosefu wa Choo .
Jengo la Choo chenye matundu 16 kilichojengwa katika Shule ya Msingi Isela ambapo ujenzi wa Shimo la maji machafu unaendelea kukamilishwa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Isela,Bi Paskazia Changaka amesema kuwa Mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa,ofisi ya Walmu,Choo cha Wanafunzi na Walimu umekamilika na fedha iliyotumika ni shillingi 66,600,000/= zilizotolewa na Serikali na wamejenga kwa kutumia mafundi ujenzi Wakazi kwa usimamizi wa Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri na Kamati ya ujenzi na ujenzi umeafanyika kwa kiwango na ubora kulingana na thamani ya fedha.
Mwalimu Mkuu huyo ameahidi kutekeleza maelekezo na maagizo ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Kamati ya Shule na kuhakikisha wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza, darasa la pili, darasa la tano na Sita wanahama na kuanza kusomea katika vyumba hivyo vya madarasa na Wanafunzi wa darasa la tatu na darasa la Nne watabaki katika Madarasa ya Shule ya Msingi Busagara na kwamba wataendelea kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa shimo la Choo cha Wanafunzi ili kiweze kukamilika mapema na kuanza kutumika lakini kwa sasa wataendelea kutumia Choo kilichopo katika Shule ya Msingi Busagara.
Mwalimu Mkuu,Bi Changaka alitoa takwimu za Wanafunzi wa Shule hiyo kwamba kuna jumla ya Wanafunzi 703 wanaosoma darasa la awali hadi darasa la saba ambao wamesajiliwa na wanaendelea na masomo kama kawaida na kwamba hali ya maendeleo ya kitaaluma ni nzuri na inaridhisha na kuwaomba ushirikiano zaidi Wananchi waweze kujitoa kuchangia shughuli za maendeleo ya Shule yao.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe, Juma Sweda (Katikati) akifanya Ukaguzi kwenye Kiwanda cha Uzalishaji wa Mawe na Kokoto cha KASKO (Kulia ni Meneja wa Kiwanda hicho Bw,Japhet Gerasa akimwelekeza na kumwonyesha Mkuu wa Wilaya namna Uzalishaji wa Kokoto na Matofali unavyofanyika
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bi, Dianah Kuboja amesema kwamba Menejimenti imesimamia kikamilifu ujenzi mwa madarasa hayo kupitia kwa Wataalam wa Ujenzi wa Halmashauri na mradi umetekelezwa kwa ubora na kiwango ambapo kanuni, taratibu na miongozo ya Shule inaafahamika na ipo wazi na Idara ya Elimu Msingi itaendelea kufuatilia utekelezaji wamiradi na shughuli zote zinazohusu Sekta ya Elimu pamoja na kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa shimo la Choo na unakamilika kwa wakati ili kuwanusuru na kuwaondolea adha Wanafunzi.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ameweza pia kukagua miradi na shughuli zinazoendelea kutekelezwa katika maeneo ya Kata ya Usagara ikiwemo Ujenzi wa Sekondari ya Kijiji cha Nyang”homango, kukagua shughuli katika Kiwanda cha Uzalishaji wa Mawe na Kokoto cha KASKO,na Nyanza Roads Works, Mradi wa Maji bomba wa Usagara, Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Usagara pamoja na Mkutano wa hadhara wa Kijiji cha Usagara.
Mataofali yanayozalishwa kwa kutumia Vumbi la Kokoto na Mawe katika Kiwanda cha KASKO cha Wilayani Misungwi.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi anaendelea na ziara ya kukagua na kuona utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo katika Kata zote 27 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi akiambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri..
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.