Mkuu wa Wilaya ya Misungwi awataka watendaji kushirikiana na Madiwani kuongeza kasi na ufanisi katika ukusanyaji wa Mapato Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Johari Samizi katika kikao cha Baraza la Madiwani robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 17, Mei,2024 ambapo amewataka watendaji pamoja na waheshimiwa Madiwani kushirikiana kwa pamoja kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Aidha Bi.Samizi amesisitiza na kukea baadhi ya viongozi ambao wanakwimisha zoezi la ukusanyaji wa mapato waache tabia hiyo mara moja kwa sababu haina afya wala tija kwa maendeleo ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
“Wakati wengine wanapigana kupiga hatua mbele kuna wengine wanatuvuta mashati hatua tano nyuma hasa waheshimiwa madiwani katika hilo mimi nakuwa mkali sana”amesema Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe.Kashinje Machibya kupitia Baraza la Madiwani amemtaka Mkurugenzi kuendelea kusimamia kikamilifu mapato na matumizi ya fedha za Halmashauri pamoja menejimenti kwa ujumla wake, na kutoa rai kwa taasisi za Serikali kuendelea kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
“Mpango wa matumizi ya fedha za Serikali ni kutotumia fedha nje ya mpango wa bajeti usimamie usiyumbishwe”amesisitiza Bw.Machibya.
Hata hivyo Bw.Machibwa ametoa pongezi kwa Meneja wa Tanesco Wilaya ya Misungwi Bw.Festo Ndemaya kwa kuwajibika kikamilifu kwa kutoa ushirikano kwa washimiwa madiwani pamoja Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na kuzitaka Taasisi zingine kuiga mfano kwa meneja huyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru amesema kwamba ataendelea kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri kwa uadilifu mkubwa ili kufikia malengo ambayo Halmashauri imekasmia ambapo mpaka sasa Halmashauri imeweza kusanya zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya ndani.
Sambamba na hilo ameongeza kuwa Halmasahauri imejipanga kuongeza Pos kadhaa ili kuongeza kasi na kuimarisha ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Wakuu wa Idara,Vitengo na wakuu wa Taasisi wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao cha Baraza la madiwani robo ya tatu 2023/2024 kilichofanyika tarehe 17,Mei,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani akifuatilia na kupitia taarifa mbalimbali kupitia vishikwambi katika mkutano wa Baraza la madiwani robo ya tatu 2023/2024 ambapo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 17,Mei,2024
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.