Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya wasichana Mwanangwa kupunguza utoro wa Wanafunzi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Veronika Kessy amezindua uchimbaji wa msingi wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wasichana Mwangwa iliyopo kata ya Mabuki Wilaya ya Misungwi amesema kuwa ni hamasa kubwa kwa jamii kuendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mabuki amesema shule hiyo ambayo itagharimu Zaidi ya shilingi milioni 700,000,000/= itasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi shuleni na kuzingatia masomo yao na kuwa hamasa ya kujisomea, hata hivyoameongeza kuwa kutakuwa na awamu ya kwanza itakayoanza na majengo 4 ambayo yatagharimu shilingi milioni 457,000,000/=likiwemo bweni la wasichana,bwalo kwa ajili ya chakula na vyumba 4 vya madarasa pamoja na ofisi za Walimu.
Mhe. Veronika Kessy ameongeza kuwa majengo hayo yanatarajiwa kukamilika Mwezi wa tisa mwaka 2022,na shule hiyo itapokea wanafunzi wa kike kutoka sehemu mbalimbali ya Wilaya ya Misungwi watakao kuwa na vigezo vya kujiunga na shule hiyo vitakavyokuwa vimewekwa.
Katika Hafla hiyo Mhe.Veronika Kessy amewashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki uchimbaji wa msingi wa Shule hiyo ya Sekondari Mwanagwa kwa kuokoa gharama za ujenzi katika hatua ya msingi ambapo fedha hiyo ingetumika kuchimba msingi badala yake itatumika kwenye matumizi mengine .Nakutoa wito kwa wananchi waendelee kujitokeza kuiunga mkono Serikali katika kushiriki shughuli za miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Bw Benson Mihayo ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kuleta fedha shilingi 475,000,000/=kwa awamu ya kwanza ambazo zinajengwa kupitia mpango wa TASAF ambazo zitatumika kujenga shule ya Sekondari ya wasichana Mwanangwa kwa ajili ya kutatua tatizo la umbali na ushawishi kwa wanafunzi wanapotembea umbali mrefu wakati wa kwenda shule,na itasaidia wanafunzi kusoma kwa ufanisi na kufaulu vizuri katika mitihani yao.
Naye Afisa Elimu Sekondari Bi Diana Kuboja amesema Shule hiyo itasaidia kupunguza umbali kwa wanafunzi wa naoishi vijiji vya mbali,ambapo kwa sasa wanafunzi wanatoka zaidi kilomita ishirini kutoka kwenye makazi hadi eneo la shule ya Sekondari Mawe matatu watafaidika na mradi huo. Sambamba hilo amesema kuwa Shule hiyo itakuwa una uwezo mkubwa kubeba wanafunzi takribani wasiopungua mia nne.
Ameongeza kuwa Shule hiyo itaanza na madarasa manne ambayo yatabeba wanafunzi wasio pungua mia mbili na bweni moja la wanafuzi litakalo chukua wanafunzi themanini.Pia shule ipo eneo sahihi kwa ajili kusaidia kupunguza umbali kwa wanafunzi wanaotoka katika kijiji cha Mwagagala na maeneo mengine.
Naye mkazi wa Kata ya Mabuki Bw.Peter Masalu amesema kuwa ujenzi wa Shule hiyo utasaidia kupunguza umbali kwa wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali ,pia itawasaidia wanafunzi kuwahi vipindi vya masomo vya asubuhi tofauti na sasa ambapo wanafunzi wengi wanachelewa vipindi kutokana na umbali uliopo.
Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya akishiriki katika uchimbaji wa msingi Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanangwa.
Diwani wa Kata ya Misungwi Mhe, Muganyizi Ferouzi (katikati) akichimba msingi katika Shule ya Sekondari Mwanangwa akiwa na baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wa Kata ya Mabuki.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.