Serikali imesitisha jaribio la Mwanafunzi wa Kidato cha tano kuodheshwa kwa Mwanaume Askari Jeshi mara baada ya kurejeshwa kwa mahali ya Milioni mbili na Nusu zilizotolewa kwa Wazazi wake Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Tamko hilo limetolewa na Mkuu wa Wiaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha katika kijiji cha Mamaye Kata ya Mamaye Wilayani Misungwi katika Familia ya Mwanafunzi Anisia Pauline Luchagula ambaye amenusurika kukatishwa ndoto zake za kuendelea na masomo ya kidato cha Tano katika Sekondari ya Bukongo Wilayani Ukerewe.
Mhe, Chacha amekemea vikali kitendo cha wazazi kukatisha ndoto na malengo ya watoto wao kimasomo jambo ambalo halikubaliki na linawanyima haki zao za msingi kama vile kupata elimu kwa ajili ya maisha yao na taifa kwa ujumla,pia ametoa mahitaji ya msingi ya kujikimu kwa mwanafunzi huyo pamoja na fedha taslimu shilingi 300,000/=.
“Baba mtu mzima mwanaume anamwita mtoto wa kike Mchumba akamatwe kabla hajaenda mbele, baadala amwite Mwanangu, mdogo wangu, lakini anajisikia fahari kumwita mchumba katoto kadogo tu ” Ameonya Mhe, Mkuu wa Wilaya, Paulo Chacha.
Mhe, Paul Chacha amesema ukaribu na Wananchi Wilayani humo umeweka urahisi wa kupokea taarifa hizo na kusema hatua zitachukuliwa Kwa mtumishi huyo na hatimaye kuagiza kufikishwa salama mwanafunzi huyo kufika Wilaya ya ukerewe katika shule aliofaulu kuendelea na masomo yake.
Mkuu wa Wilaya huyo ametoa Rai kwa wazazi kuhakikisha wanatimiza majukumu yao na kuacha mara moja vitendo vya kuwaodhesha watoto wakiwa masomoni ni jambo ambalo ni kinyume na Sheria , na taratibu za nchi na ukatili dhidi ya watoto.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Misungwi, Bi Aziza Mangu amesema kitendo kilichotokea cha kutaka kukatishwa masomo hakikubaliki katika jamii hivyo kupitia jitihada za uongozi wa Wilaya hatutarajii tena kitendo kama hicho kutokea kwa wanafunzi wengine na kuiomba jamii kubadilika.
Afisa Elimu wa Kata ya Igokelo Wilaya ya Misungwi Bw. Hashimu Zaidi akimwakilisha Afisa Elimu Sekondari amesema kwamba mwanafunzi huyo amekuwa na maendeleo mazuri na ufaulu wa dalaja la pili katika mchepuo wa sayansi katika masomo ya Kemia,Biolojia na Jiografia (CBG) na ni miongoni mwa Watoto 6 waliofanya vizuri hivyo kitendo hiki hakivumiliki na hatutokubali anatakiwa kuendelea na masomo yake ya kidato cha tano bila kukatishwa ndoto zake .
Wakati huo huo, Baba Mzazi wa Alisia Bw. Pauline Luchagula ameomba radhi kwa kitendo cha kutaka kumuodhesha binti kinyume na sheria na kanuni za nchi hivyo amekiri kutokutokea tena kwa kitendo hicho na kutoa wito kwa familia zingine zijifunze kupitia familia yake kwa watoto wao na iwe fundisho kwa familia zingine za hapo kijijini na ndugu na jamaa.
Naye, Mama Mzazi wa binti hyuo Bi. Maria Ng'aya Mama mzazi wa mwanafunzi huyo alikiri kutokea kitendo hicho ambapo amesema jambo hilo walilifanya kwa kutotegemea na hawakulazimishwa bali walifanya bila kukusudia na kuushukuru uongozi kwa kuingilia suala hili na amesema mwanaye sasa aende akasome na hatorudia tena.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha akimwaaga Mwanafunzi Bi Anisia Pauline Luchagula chini ya usimamizi mkali wakati akielekea Wilayani Ukerewe kwa ajili ya Masomo yake hivi karibuni,ambapo DC alimkabidhi Fedha taslimu shilingi 300,000/= pamoja na mahitaji mengine ya kujikimu.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.