Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Johari Samizi aendelea na Ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi na kutoa hamasa kwa Wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza..
Akiwa katika ziara katika Kata ya Usagara iliyofanyika tarehe 5 Novemba 2024 Mhe. Samizi ametembelea na kukagua maendeleo katika Kituo cha Afya Usagara ambapo wameanzisha Ujenzi wa Jengo la Mionzi na tayari boma limekamilika kupitia nguvu na juhudi za michango ya Wananchi wa Kata hiyo na umuhimu wa kuboresha huduma za afya kwa Wananchi na kuelekeza ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati ili Wananchi waweze kupata hudumu bora za afya pamoja na ukaguzi wa mradi wa Wawekezaji wa ndani wa Ujenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha TANUKU Africa LTD cha Nyashishi kilichojengwa kwa shilingi Bilioni 1.5 na kinachotarajia kutoa ajira kwa Wananchi wazawa wa Wilaya ya Misungwi na kuwasihi kuendelea kutunza usaafi wa mazingira Kiwandani hapo.
Mhe. Samizi amewataka Wananchi wa Kata ya Usagara kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali na kuna kila sababu ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora na kuimarisha uchumi wa familia na jamii kwa ujumla, na kuwahakikishia Wananchi ambao wanasubiri malipo ya fidia ya upanuzi wa Barabara kuu kuwa na subira Serikali inakamilisha utaratibu wa malipo hayo na watapatiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria.
Naye Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Misungwi Bi. Elly Makala amewasihi Viongozi na Watendaji wa Kata ya Usagara kufanya kazi wa uadilifu na kuhakikisha wanazingatia taratibu, kanuni na sheria za shughuli za ujenzi kwa kufuata sheria za manunuzi pamoja na kutoa stakabadhi za malipo kwa michango ya maendeleo ya ujenzi inayotolewa na Wananachi ili kuzingatia utawala bora na utawala wa sheria kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi anaendelea na ziara ya siku tatu ya kukagua miaradi ya maendeleo kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 7 novemba 2024 pamoja na kusikiliza na kutatua kero zaWananchi Wilayani Misungwi ikiwa na kutoa hamasa kwa Wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024, ametoa wito kwa Wananchi wote waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura na kuwachagua Viongozi wanaowataka kwa ajili ya kuleta maendeleo ambapo Kauli mbiu ya Uchaguzi mwaka 2024 ni “Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi Novemba 27, 2024”.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.