Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi akabidhi Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Wanafunzi na Watoto wenye ulemavu kutoka Shule za msingi 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza..
Akizungumza Tarehe 21 Mei, 2025 katika Viwanja vya Shule ya msingi Mitindo katika hafla ya makabidhiano ya Vifaa saidizi ,amesema kwamba amefurahishwa sana na Shirika la Sense International linalofanya kazi Wilayani Misungwi na Wilaya ya Shinyanga Vijijini kupitia mradi wa Elimu Jumuishi (TO51) ambalo limetoa vifaa saidizi kwa Watoto wenye mahitaji maalumu na vitawasaidia kufika shuleni ili kufanikisha ujifunzaji pamoja na Jezi na Mipira kwa Wanafunzi wanaosoma katika Shule 16 zinazotekeleza mradi huo na kuwapongeza kwa juhudi za kuanzisha Vikundi vya Wazazi wa Watoto wenye ulemavu kwa ajili ya kuwakopesha kupitia vikundi na tayari Vikundi 13 vimeshapatiwa mtaji wa shilingi Milioni 6,500,000/= kutoka Halmashauri ili kuweza kuwainua kiuchumi na kuwaongezea kipato cha familia.
Mhe. Samizi amesema na kuwaelekeza Watoto na Wazazi hao kuvitunza, kuvilinda na kuvitumia vizuri vifaa saidizi hivyo ili viwawezeshe kuboresha na kuimarisha taaluma na hatimaye kuongeza ufaulu kwa Watoto hao wenye mahitaji maalum na kuwapa manufaa kupitia sekta ya elimu na kukuza uchumi katika familia na kutoa wito kwa jamii kutowaficha Watoto wenye ulemavu hivyo, wawapeleke shule ili waweze kupata elimu.
Akiwasilisha taarifa ya mradi wa Elimu Jumuishi Mratibu wa Mradi huo kuptia Shirika la Sense Intenational Bw. Gerald Tuppa amesema kuwa mradi huo umeanza kazi mwaka 2022 katika Shule 16 zilizopo katika Kata 3 za Mwaniko, Mabuki na Misungwi na tayari umefanikiwa kutoa mafunzo kwa Walimu wa Elimu jumuishi ya namna ya kuwabaini Watoto na tayari wamebaini Watoto wenye mahitaji maalum 1,000 kutoka Wilaya za Shinyanga vijijini na Misungwi katika Mikoa miwili iliyopo kwenye Mradi, sambamba na ugawaji wa Vifaa saidizi vya Vitimwendo 15, Jezi na Mipira kwa Watoto wenye ulemavu kwenye Shule hizo 16 Wilayani Misungwi.
Kwa upande wake Afisa Elimu Maalum Wilaya ya Misungwi Bw. Charles Pamba amewashukuru Shirika la Sense International kwa utayari wao wa kusaidia kupitia Mradi huo wa elimu Jumuishi na vifaa saidizi hivyo vitasaidia watoto hao kumudu masomo kikamilifu na kuiomba jamii kuendelea kuwatoa watoto wenye ulemavu ili wasome na kupata elimu kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.