Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Johari Samizi, ametoa wito kwa Wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka Watoto Shule kwa ajili ya kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2024 na kutoa malezi bora kwa Watoto hao ili kulinda mila na desturi za jamii, pamoja na kukuza maadili mema nchini.
Ameyasema hayo tarehe 7 Novemba 2024 katika ziara yake ya kukagua, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ambapo katika kikao na wananchi wa Kata ya Mondo, Mhe. Samizi ameeleza kuwa malezi bora ni msingi wa kuzuia vitendo viovu vinavyoweza kuathiri maendeleo ya watoto na jamii kwa ujumla ambapo Wazazi wanapaswa kuwa mfano mzuri kwa watoto wao, kwa kuwafundisha maadili na tabia njema ambazo zitawasaidiA kuwa raia wema na wenye mchango chanya katika jamii pasipo kufuata vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vile kuwaozesha wakati bado wanasoma.
Mhe. Samizi ameongeza kuwa jamii ina jukumu kubwa katika malezi ya watoto, na hivyo ni muhimu kwa wazazi na walezi kushirikiana na viongozi wa jamii katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora ambapo jamii kuimarisha ushirikiano katika kutokomeza vitendo vya ukatili kijinsia unyanyasaji na uhalifu, ili kuweza kujenga mazingira salama kwa watoto, sambamba ha hilo amewataka Wananchi Wilayani humo kutumia mvua hizi zinazonyesha kulima mazao yanayostahimili ukame kutokana na mwenendo wa mvua kwa mwaka 2024 pamoja na kujiandaa kikamilifu kushiriki katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 na kutumia haki ya kikatiba ya kuchagua mtu wanayemtaka katika eneo lao.
Katika hatua nyingine Mhe. Samizi amekagua nyumba ya Mtumishi ambayo ipo katika hatua ya ujenzi wa msingi pamoja na ukamilishaji wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mondo na kumtaka Mtendaji wa Kata kuhakikisha anasimamia ipasavyo utekelezaji wa ujenzi huo kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za manunuzi na kwamba Fundi ujenzi aweze kukamilisha Jengo la Nyumba ya Mtumishi kwa muda uliopangwa wa siku 60 ili Wananchi wapate huduma bora za afya.
Naye Mtendaji wa Kata ya Mondo Bi. Byasi Kasuguli wakati akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa nyumba ya Mtumishi amesema kuwa shilingi Milioni 92.6 zimetolewa kupitia mpango wa TASAF kwa ajili ya ujenzi huo ambao ulianza tarehe 16 Oktoba 2024 kwa kushikisha nguvu na mchango ya jamiii pia aliahidi kutekeleza na kusimamia mradi wa ujenzi huo kikamilifu ili Wananchi waweze kunufaika na huduma hi
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.