Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi aagiza Baraza la Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukusanyaji wa Mapato ya Ndani shilingi Bilioni 4,704,013,000/=kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhe, Johari Samizi amesema kwamba hakuna nchi wala Halmashauri inayoweza kuendeshwa bila kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaimarika , na siyo tu kukusanya na kuhakikisha kwamba yanatumika ipasavyo, na amesisitiza Idara zote zinazohusika na ukusanyaji wa mapato kuweka mikakati madhubuti, kwamba tumeanza mwaka mpya wa Serikali, hivyo idara zinazohusika zikusanye mapato kwa uaminifu na kwa uadilifu na mapato haya yakatumike kuwaletea maendeleo Wananchi kama ambavyo Serikali imekusudia.
“Amesema hatarajii kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 kuwa mkusanya mapato kukaa na fedha ya Serikali bila kupeleka benki zaidi ya masaa ishirini na nne (24) endapo itatokea hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake” Alisisitiza DC Johari Samizi.
Mhe,Johari Samizi amewawasistiza Viongozi na Watendaji wawe na vipaumbele vya kufanya mabadiliko ya vifungu vya matumizi katika shughuri za maendeleo tu na sivinginevyo na kuendelea kutekeleza miradi kikamilifu pia amewataka Wananchi kuachana na shughuli zote za kibinanadamu katika vyanzo vya maji na maeneo tengefu ili kuimarisha usalama wa mazingira na kuepuka mabadiriko ya tabia ya nchi kwa ujumla na kusisitiza matumizi ya Nishati mbadala ya kupikia.
Mhe, Mkuu wa Wilaya huyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mabadiliko makubwa kuliko awamu zote na kujenga na kukamilisha miradi mingi na mikubwa katika Wilaya ya Misungwi ikiwemo Chuo cha Uhasibu TIA Usagara na kueleza kuwa kufikia mwezi Disemba 2024 miradi yote itakuwa imekamilika ikiwemo Daraja la JPM la Kigongo –Busisi pamoja na kuwataka Wananchi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikari za mitaa mwaka 2024 kwa kuboresha Daftari la kudumu la Wapiga kura na kupata haki ya kumchagua kiongozi anayempenda kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe, Machibya ameeleza kwamba Baraza la Madiwani halitokuwa tayari kumvumilia Kiongozi ama mfanyabiashara yoyote atakaye sababisha na kuleta ukwamishaji katika suala la Ukusanyaji wa Mapato kwa kuzingatia kipaumbele cha Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni Mapato, Mapato na Mapato ili kuweza kupeleka asilimai 40 za mapato katika kutekeleza miradi ya vijijini.
Mhe, Machibya amesema kwamba Baraza la Madiwani lina wajibu wa kusimamia mapato ya ndani kwa bidii kwa maslahi mapana ya Wananchi na kuhakikisha kutokutoa mwanya wa upotevu wa mapato kwa namna yeyote ile na kuwataka Watendaji wa Kata kuendelea kusimamia na kutumia kikamilifu fedha za Miradi ya Maendeleo ili ziendane na thamani ya fedha katika miradi husika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi Mhe, Emmanuel Masangwa ameipongeza Halmashauri kupitia Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watendaji wote kuhakikisha wanasimamia fedha za Miradi ya maendeleo kwa umakini mkubwa ili kuwaletea maendeleo Wananchi na kuwaomba Viongozi pamaoja na Watendaji kuongeza ushirikiano katika kuwaletea Wananchi maendeleo ya dhati.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw.Addo Missama amemshukuru Mhe, Rais kwa kumteua na kuwaomba Madiwani, Watendaji kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza shughuli za Serikali na kutimiza malengo yaliyowekwa na kuahidi kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria ili kuweza kuwaletea maendeleo Wananchiwa Wilaya ya Misungwi.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani Misungwi wakiwa katika kikao Cha Baraza robo ya Nje Mwezi Julai 2024
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.