Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe, Paul Chacha akagua Miradi ya Maendeleo na kuhimiza kukamilika kwa wakati Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paul Chacha katika ziara yake ya kukagua na kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali February 26,2023 ukiwemo Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya uliopo kata ya Nhundulu,mradi wa Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya Awali na choo matundu 6 katika Shule ya msingi Mwawile,Mradi wa barabara ya changarawe km 7 Mawemabi Kata ya Mwagiligili,Mradi wa Maji kata ya Mbarika,Mradi wa Umeme Vijini REA ,Mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya wasichana Mwanangwa na Uendelezaji wa Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Misungwi ambapo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kujituma na hivyo kuwaletea Wananchi maendeleo.
Amesema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kukugua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo ameagiza kufanyike kwa marekebisho katika milango katika Kituo cha Afya Mwawile na kuharakisha kuwekwa kwa huduma Umeme kwa wakati katika kituo hicho.Hata hivyo wakati wa ziara hiyo pia ametoa maelekezo kuhusu kufanyiwa kwa marekebisho ya baadhi ya viti vya kukalia wanafunzi wa Awali ili kuondoa usumbufu wakati wa kujifunza.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi,Mhe,Petro Sabato amewataka watalaam kutumia nafasi walizo nazo kwa uaminifu mkubwa ,kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kuwapa wananchi huduma bora na stahiki ili kutimiza dhima ya Serikali ya awamu ya sita kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bw, Clement Morabu amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ilipokea fedha shilingi 500,000,000 /=kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa awamu ya kwanza ikiwa maelekezo ya Serikali kwa kujenga majengo mawili (OPD na Maabara) Mwaka wa fedha 2020/2021ilipokea fedha shilingi Bilioni moja fedha hizo zilitumika kujenga majengo 5 Jengo la Utawala,Dawa,Mionzi,kufulia na Jengo la Mama na mtoto.
Vilivile Dkt Morabu aliongeza kuwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ilipokea fedha shilingi 800,000,000/= kwa ajili ya kujenga Wodi ya wanaume upasuaji,Wodi ya wanawake upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti( Mortuary), 2022/2023 ilipokea shilingi 750,000,000/=kwa ajili ya kujenga Wodi ya watoto,Wodi ya magonjwa ya ndani wanawake na Wodi ya magonjwa ya ndani wanaume na Mortuary.
Naye Injinia wa Maji Bw.Marwa Kisibo ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Misungwi alieleza kwamba Mradi wa maji Mbarika Misasi ulianza kutekelezwa mwaka 2014/15 na kusafiwa Mwaka 2012 kwa lengo la kuwahudumia watu 41,591 katika Vijiji vya Lutaletale,Bugisha,Ngaya ,Ikula ,Sumbugu,Matale,Kasolol,Nduha ,Isuka,Manawa na Misasi.Hata hivyo alifafanua kuwa shughuli kuu zilizopangwa na kufanyika katika mradi huo ni kujenga njia kuuya kusafirisha maji mita 11,235( km 11.235),kujenga mtandao wa kusambaza maji mita 5864 ( km 5.864) na kujenga mtenki 2 yenye mita ya ujazo 45 katika Vijiji vya Mbarika, Lutalutale na Bugisha, ambapo watu 15,042 watanufaika kwa kupata maji safi na salama.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha wa kwanza kulia akimbatana Viongozi mbalimbali na Wataalam wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo kituo cha Afya Mwawile February 26,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha akikagua madawati katika Shule ya Msingi Mwawile juzi wakati wa ziara yake,ambapo alitoa maelekezo ya kurekebishwa kwa baadhi ya madawati ambayo yalikuwa na dosari.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha akimpa mkono Mkazi mmoja wa Kijiji cha Igongwa ambapo alimwahidi kumlipia gharama zote ya kuingiza Umeme katika nyumba yake pamoja na familia yake wakati akikagua Mradi wa uunganishaji wa umeme Vijijini REA katika kijiji cha Igongwa.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.