Mkuu wa WIlaya ya Misungwi, Juma Sweda azindua na kufungua Bweni la Wasichana lililogharimu kiasi cha shilingi Milioni 120 katika Shule ya Sekondari Misungwi, Mkoani Mwanza
Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la ufunguzi wa bweni hilo Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda amesema na kupongeza uongozi wa Sekondari hiyo kupitia kwa Mkuu wa Shule hiyo ambaye amekuwa mstari wa mbele na ameonyesha kwamba ni mchapakazi na mwenye moyo wa kupenda maendeleo ya jamii na siyo mtu wa kufanya mambo binafsi na kujinufaisha ndio sababu amefanikiwa na kukamilisha ujenzi wa bweni baada ya kubana matumizi mbalimbali ya shule ikiwemo Chakula.
Ameeleza kwamba bweni hilo litaleta na kuongeza chachu ya kusoma kwa Wanafunzi na kuwataka wanapomaliza wasisahau Wilaya ya Misungwi na kuendelea kuikumbuka daima katika maisha yao, hivyo jukumu kubwa sasa baada ya kukamilika kwa bweni ni kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu katika Mitihani.
“ Hili ni bweni ambalo kimsingi ni bweni la mfano unaweza ukaangalia hata Mkoa wa Mwanza bweni kama hili unaweza usilpate ni bweni ambalo lina facilities zote na ni bweni la kisasa sana ” Alisema kwa kusisitiza Juma Sweda.
Juma Sweda amewahakikishia Wanafunzi hao wa Kidato cha tano na sita kwamba Serikali itaendelea kuboresha miundombinu na mazingira yao na kuwawezesha kusoma vizuri ili kuongeza ufaulu zaidi na kuwaomba kulitumia vizuri bweni hilo zuri ambalo lina mahitaji yote yanayopaswa kuwepo bwenini na ni la kisasa zaidi.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Misungwi, Ananius Mbandwa ameeleza katika taarifa ya mafanikio ya shule hiyo kwamba Shule hiyo imeanzishwa mwak 1994 na kufanikiwa kunza Kidato cha tano mwaka 2016 katika mchepuo wa EGM na CBG
Akifafanua zaidi katika suala la ujenzi wa bweni hilo uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 120 na laki tano hadi kukamilika ambapo fedha zilizotumika ni fedha shilingi Milioni 40 ya mapato ya ndani ya Sekondari hiyo ambayo imetokana na bakaa na bana matumizi ya fedha ya Chakula kwa Wanafunzi na fedha shilingi Milioni 60 ambayo ni kutoka Serikali kuu kupitia Wiazra ya Elimu
Bw, Mbandwa ameeleza na kufafanua kwamba bweni hilo lina uwezo wa kukaa vitanda 40 vya aina ya Deka kwa Wanafunzi zaidi ya 80 ambapo kwa sasa litatumiwa na Wanafunzi zaidi ya 80 ambao ni 50 wa Kidato cha sita na 30 wa Kidato cha tano waliopo kwa mwaka huu 2020/2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Kisena Mabuba amewapongeza Viongozi wa Shule ya Sekondari Misungwi kwa ushirikiano na juhudi za makusudi za kuleta mabadiliko ya elimu wanazoendelea kuzifanya hususani katika matokeo ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne na Sita kwa hakika Wanafunzi hawa wanaendelea kupindua meza kibabe tu.
Mwonekano wa bweni la kisasa la Wasichana lilojengwa na kukamilika katika Shule ya Sekondari Misungwi linaloweza kubeba Wanafunzi 80 wa Kidato cha tano na sita , bweni hilo limegharimu shilingi Milioni 120 tu fedha za Serkali.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda (katikati) akikata utepe kuashairia ufunguzi rasmi wa Jengo la bweni hilo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Kisena Mabuba wa kwanza kushoto akifuatiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Petro Sabatto na Afisa Elimu Sekondari Diana Kuboja pamoja na Walimu na Wanafunzi wwa Kidato cha tano na sita.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda akiangalia na kukagua eneo la kunawa mikono katia moja wapo ya bafu ndani ya Jengo la bweni la Wanafunzi katika Sekondari ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.