Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha aagiza TAKUKURU Wilaya ya Misungwi kuchunguza miradi 4 ya ujenzi wa barabara iliyobainika kujengwa chini ya kiwango Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha katika ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya Nyashishi hadi Fella yenye urefu wa kilomita 8 inayojengwa na Mkandarasi Lukambo Contractors Co. LTD ya Bunda ambapo ujenzi wake unaendelea kwa kusuasua wakati Wakala wa barabara mjini na Vijijini Wilayani Misungwi wameonyesha kushindwa kusimamia kikamilifu na kusababisha malalamiko kwa Wananchi na jamii inayotumia barabara hiyo.
Mhe, Chacha ameelekeza na kusisitiza Meneja wa TARURA Wilaya ya Misungwi kusimamia kikamilifu ujenzi wa mradi huo na kuhakikisha wananchi hawakwami wakati wa kutumia barabara hiyo hususan kipindi cha msimu huu wa mvua na kuagiza Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Misungwi, kuchunguza miradi hiyo kwa kuwapekua wote Meneja wa TARURA atoe nyaraka zote alizoficha na kumhoji Mhandisi aitwae Hosea aliyetajwa kupewa fedha Tsh, Milioni 15 kutoka kwa Mkandarasi ili kuziba midomo ya Wananchi kufuatilia na kujiridhisha na ujenzi huo na kubaini mapungufu ya ujenzi wa barabara hizo na kutoa mapendekezo kwa mamlaka husika kuhusu Mwenendo wa Mkandarasi huyu ambaye anapewa kujenga barabara nyingi wakati huo hazitekelezi kwa wakati.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Bw. Abdi Makange amewakumbusha Watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheriana taratibu pia kutumia vyema Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia Bunge mwaka 2021 na kuwaasa Watumishi kufanya kazi kwa weledi na ubunifu
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilayaya Misungwi Mhe. Kashinje Machibya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Usagara ameeleza namna ambavyo miradi inavyosussua ikiwemo ya ukarabati wa barabara ambayo imekua ikileta adha kwa wananchi na kusema kuwa hakuna kiasi fedha kitakachopotea kwa mradi wowote utakaokua na kasoro hivyo hatua zimeshachukuliwa kama alivyo agiza Mkuu Wa Wilaya ya Misungwi
Baadhi ya Wananchi na Wakazi wa maeneo hayo wamesema na kukemea vitendo vya Baadhi ya watumishi kutenda kinyume na maadili yao na kuwataka wazingatie na kufuata maelekezo ya serikali ili kutimiza majukumu yao hivyo kupitia elimu ndio njia ya kuimarisha maendeleo na sio kinyume.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha akikagua Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Nyashishi hadi Fella Wilayani Misungwi yenye urefu wa km 8 ambapo alimbatana Viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe ,Paulo kushoto,katikati ni Mwenyeki wa Halmashauri ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya na upande wa kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Bw,Abdi Makange wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya Ujenzi wa Barabara Nyashishi hadi Fella 27,Septemba,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha akipima upana na kimo wa mtaro wa maji katika barabara ya Nyashishi hadi Fella yenye urefu wa km 8 hivi karibuni ambapo alitoa maelekezo kukamilika kwa wakati kwa mradi wa ujenzi huo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.