Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe,Juma Sweda atatua Mgogoro wa Wachimbaji wa Madini na kuagiza kupitiwa upya kwa Mkataba wa Uchimbaji Madini baina ya Kikundi cha Nyabayombe na Ushirika pamoja na Kampuni ya Seif Mahumbi kwenye Mgodi wa Madini ya Dhahabu wa Kijiji cha Lubili Wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza.
Akizungumza na baadhi ya Viongozi na Wachimbaji wadogo wadogo katika Mkutano uliofanyika katika maeneo ya Machimbo ya Nyabayombe, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Mhe,Juma Sweda amewataka Wachimbaji ambao ni Wanakikundi cha Nyabayombe na Wanaushirika kushirikiana na kufanya mapitio upya ya Mkataba wa shughuli za uchimbaji walioingia na Mwekezaji wa Kampuni ya Seif Mahumbi na kuweka vizuri makubaliano ili uweze kunufaisha upande wote kutokana na mapato yatokanayo na Madini ya Dhahabu.
Mhe,Juma Sweda amewataka pia Viongozi wa Ushirika na Kikundi cha Nyabayombe kufanya kazi na kuwajibika ipasavyo kwa Wanachama na kutetea maslahi yao na kuachana na mambo ya kurubuniwa na kudaganywa na Watu wengine wasiowatakia mafanikio mema na hatimaye kuwapotosha na kuwaomba Wanaushirika na Wanakikundi kuendelea kuheshimu Viongozi waliopo madarakani na kuwapa ushirikiano wa kutosha.
Alisema na kusisitiza kwamba,eneo hilo la uchimbaji litabaki na Wamiliki wenye Leseni 16 za Wachimbaji wadogo wadogo kupitia Kikundi cha Nyabayombe ambao ndio Wamiliki wa Mgodi huo na kupiga marufuku Kikundi cha MIMICOSO kutojihusisha na shughuli za Uchimbaji katika Wilaya ya Misungwi kutokana na kutosajiriwa na kutumika vibaya Kinyume na Kanuni na taratibu.
Naye, Mwenyekiti wa Ushirika Bi,Magreth Sayi alisema kwamba wanakikundi waliamua kutafuta Mwekezaji na kumpata Bw,Seif Mahumbi ambaye waliingia naye Mkataba wa malipo ya asilimia 30 kwa 70 na kukubaliana kulipia Leseni ya Uchimbaji baada kumaliza muda wake ambapo Uongozi wa Wanaushirika na hauna ushirikiano na mahusiano mazuri na Uongozi wa Kikundi cha MIMICOSO ambacho kilianza kutafuta Mwekezaji mwingine tofauti na Bw,Seif Mahumbi bila ridhaa ya Wanakikundi na Wanaushirika wa Nyabayombe na kusababisha Mgogoro uliotokea hadi Shughuli za Uchimbaji kusitishwa na Ofisi za Madini za Kanda ya Mwanza.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.