Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,Juma Sweda ameagiza Wananchi wote Wilayani humu kulima Zao la Pamba na Mtama kwa kila Kaya kuanzia Hekari moja na Zaidi ikiwa ni mpangoa wa Kutokomeza Njaa kwa Wananchi .
Mkuu wa Wilaya huyo,amewataka Wananchi Wilayani humu kutekeleza hayo waakati wa Ziara ya kikazi aliyoifanya ya kutembelea Vijiji vyote 113 vya Wilaya kwa lengo la kuhamasishaKilimo cha Pamba na Mtama ambayo nia mazao yanayostahimili Ukame.
Juma Sweda amewataka Wananchi na Watumishi wa ngazi zote waliopo katika wilaya hiyi kulima Pamba na Mtama ili kupunguza na kuondokana na tatizo la njaa Wilayani Misungwi ambapo inakadiriwa kuwa Wilaya ina jumla ya Wananchi 351,607 na kaya 30,420 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 .
Amesema kwamba Wananchi wanatakiwa kuimarisha na kukuza Uchumi wa taifa kupitia Kilimo cha Pamba kutokana na Zao la biashara kuwa na thamani na wakulima sasa wanaweza kupata fedha kama kipato cha familia na kuwezesha kununua mahitaji mbalimbali ya familia na kuachna na tabia ya kuuza Chakula,kama Mihogo,Mahindi,Mpunga,na mengine pamoja na Mifugo ikiwemo Ng'ombe na Mbuzi hivyo wahakikishe kila Kaya inalima Mazao hayo.
Amepiga marufuku mambo na tabia ya baadhi ya Wakulima ya kuuza Chakula kikiwa mashambani na kuonya na kuwataka kuacha mara moja tabia hiyo na keleza kuwa Serikali itawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani kutokana na kuwa chanzo cha matatizo yanayosababisha upungufu wa Chakula kwa Wananchi na kuwaomba wanapopata mavuno wauze mazao yao kwenye magulio,minada na masoko yaliyopo katika vijiji vyao.
Amewataka Maafisa Ugani wa kata 27 na Vijiji 113 vya Wilaya hii kushirikaiana na Watendaji wa Kata na Vijiji kuhamasisha na Kuwaelmisha Wananchi kuhusu kilimo cha Pamba na Mtama pamoja na kuwatembelea na kukagua mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya kuzingatia na kutumia kilimo bora na cha kisasa na kinachozingatia kanuni za kilimo.
Ameaagiza Watendaji wa Vijiji kuhakikisha wanaanzisha na kuunda kikosi kazi cha kijiji cha Wakulima wa Pamba ambacho kitahusika na kuratibu na kufuatilia shughuli zote za kilimo hicho kwenye ngazi ya kijiji na kutao mapendekekezo na maoni nakuyawasilisha wilayani ili kuweza kutatuliwa na Kikosi kazi cha Wilaya pia waorodheshe Wakulima wote kwenye Daftari maalum la Wakulima wa Pamba watakaolima msimu huu na kupata takwimu sahihi za Wakulima wa Pamba na kurahisisha utoaji wa mbegu na Pembejeo na madawa ya Pamba.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.