Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Kisena Mabuba akifuatiwa ( kulia) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Warioba Sanya wakifuatila mjadala wa Uwasilishaji wa Hoja za CAG katika Mutano wa Baraza la Madiwani.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe Juma Sweda aagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri kuwachukulia hatua za Kinidhamu na kisheria Watendaji waliokusanya fedha za Mapato na hawajawasilisha Benki katika Akaunti ya Halmashauri.
Mkuu wa Wilaya huyo ametoa agizo hilo katika Mkutano wa Baraza Maalum la Hoja wakati akizungumza na Madiwani pamoja na Watendaji akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,John Mongela na kuwataka Madiwani wa Halmashauri kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria Watendaji wote ambao wameshindwa kuwasilisha benki fedha za mapato walizokusanya ambazo zilibainishwa katika Hoja za Ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2016/2017.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Misungwi (Hayupo Pichani) wakati wa Mkutano maalum wa Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Maalum ya Mitindo.
Alieleza kwamba Madiwani sasa wasimamie vizuri suala la ukusanyaji wa Mapato ili kuweza kuzuia na kuondoa mianya ya upotevu wa mapato ya Halmashauri na kuwezesha kukusanya kwa kiwango cha asilimia 100 kulingana na bajeti ya Halmashauri na kuhakikisha vyanzo vyote vya mapato vinakusanywa ipasavyo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Warioba Sanya alisema kuwa Serikali ina lengo la kuondoa hoja za ukaguzi katika Halmashauri zote nchini hivyo ni jukumu la Watendaji kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia taratibu,sheria na kanuni na kufuata miongozo ya kiutumishi na kuwataka Madiwani kusimamia kikamilifu utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Mhe,Antony Bahebe Masele (Aliyesimama) akisisitiza kuhusu utekelezaji wa Maagizo kwa Madiwani wakati akifunga Mkutano wa Baraza Maalum la Hoja
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.