Mkuu wa Wilaya ya Msungwi Mhe, Paulo Matiko Chacha ahimiza unyenyekevu na ushirikiano kwa Watumishi katika utendaji kazi na kuwatumikia Wananchi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza
Hayo yamebainishwa mapema leo katika hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Veronika Kessy ambaye amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi kwa sasa Mhe, Paulo Matiko Chacha ambapo amesema anapenda kuona Watumishi wanyenyekevu,wenye kujituma katika kazi kuwatumkia Wananchi ili kuleta Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
Ameongeza kuwa yuko tayari kuendelea kusimamia kikamilifu Miradi yote ya maendeleo aliyokabidhiwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ikiwemo Miradi ya Maendeleo ya Kimkakati ya Daraja JPM Kigongo- Busisi na Mradi wa Reli SGR ambayo Serikali imetoa fedha nyingi katika kuendeleza na kukamilisha miradi hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa Upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Veronika Kessy kwa sasa Mkuu wa Wilaya ya Iringa ameeleza anaamini Mkuu wa Wilaya aliyemwachia kijiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ataendeleza yale yote yaliyo mazuri ikiwemo katika kusimamia Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Miradi Mikubwa ya kimkakati ya Daraja la JPM na SGR pamoja na Miradi mingine ya Afya,Elimu,Maji na Umeme vijijini(REA) na kuwatakaWatumishi wampe ushirikiano katika utendaji kazi wake.
Mhe, Veronika Kessy ameeleza na kuwashauri Viongozi wa dini kuhimiza wazazi kuwapeleka shule watoto wa kidato cha kwanza kwa wakati ili kuwapa fursa watoto kupata elimu kwani ni haki yao ya msingina badala yake kuacha kuendelea kuwaficha na kuwaozesha ambapo ni kosa kisheria.
Katika Hafla hiyo Mhe.Veronika Kessy amewashukuru Viongozi na Watendaji kwa ushirikiano waliouonyesha kipindi cha Uongozi wake,kuwaomba waendelee na Moyo huo na kumpa Ushurikiano Mkuu Wilaya ya Misungwi Mhe, Matiko Paul Chacha katika kuendeleza gurudumu la Maendeleo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Bw Benson Mihayo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe,Veronika Kessy kwa Ushiriano wake kipindi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi kwa kumpokea na sasa anakwenda katika Halmashauri nyingine na kumtakia kila kheri huko aendako na ataendelea kuaendeleza yale mazuri aliyoacha ikiwemo kusimamia Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Wilaya , Ujenzi Vituo vya Afya vya Usagara na Mwawile pamoja na miradi ya ujenzi wa Madarasa katika shule za Sekondari.
Wakati huo huo mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Amani Wilaya ya Misungwi Katekister Leonidas Mtawala akitoa neon la shukrani amewaomba Watumishi na Viongozi kutoa ushiriano kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Matiko Chacha ili kuleta ufanisi mkubwa katika utendaji kazi, na kumwomba Mkuu wa Wilaya huyo akihitaji Ushauri kwa Wazee wapo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Matiko Chacha akikabidhiwa Ofisi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe,Veronika Kessy katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi leo mapema.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Matiko Chacha na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe,Veronika Kessy wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na kamati ya Ulinzi na Usalama.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakisikiliza kwa makini katika hafla fupi ya makabidhiano ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Matiko Chacha na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe,Veronika Kessy mapema leo.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.