Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi awataka Wakuu wa Idara na Watendaji wa Kata kufanya kazi na kutatua kero na migogoro ya Wananchi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhe Johari Samizi amebainisha hayo mapema leo wakati wa Kikao cha kujitambulisha mara baada ya kuanza kazi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Mhe, Johari Samizi amesema kwamba Watendaji na Wakuu wa Idara na Vitengo waendelee kufanya kazi na kutatua kero na matatizo Kwa Wananchi ikiwemo migogoro ya Ardhi, Mashamba na kero zingine.
“Ulifanya kazi kupata hivyo Usione kazi kufanya kazi Kwa bidi” Alisisitiza Mhe DC Johari.
Ameongeza kwamba Watendaji na Viongozi Wahakikishe wanakukusanya Mapato ya ndani ya Halmashauri kutokana na Taarifa za mapato hayo hadi sasa ni asilimia 56 hivyo amewaomba kuongeza juhudi katika kusimamia ukusanyaji wa Mapato ili kufikia lengo la asilimia 100 na kueleza kwamba Halmashauri zipo kwa ajili ya kukusanya Mapato kwa Maendeleo ya Wananchi.
Amewataka pia kuendelea kusimamia miradi ya Maendeleo kikamilifu ikiwemo miradi ya sekta ya elimu, Afya, Miundombinu pamoja na kusimamia na kuhakikisha utoro kwa Wanafunzi unatokomezwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Bw.Abdi Makange amewakumbusha Watumishi Wote kuendelea kufanya kazi na kuzingatia Nidhamu na kuheshimiana pamoja na kuendelea kufanya maaadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kuvaa maavazi kulingana na Waraka wa Mavazi namba 5 kwa Watumishi wa umma.
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Christopher Legonda amewataka Watendaji kuongeza juhudi na kutoa Ushirikiano katika Ukusanyaji wa Mapato kwa kuzingatia taratibu na sheria za Halmashauri na kuhakikisha wanahamasisha wamiliki wa POS Mashine wanàpeleka fedha za makusanyo Benki kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe Johari Samizi akiongea na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Makao Makuu leo mapema katika ukumbi wa Halmashauri ambapo amewataka Watumishi kufanya kazi kwa bidii ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Wakuu wa Idara,Vitengo na Watendaji wakiwa makini kusikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mpya Mhe.Johari Samizi katika kikao cha kujitambulisha kwa Watumishi wa Halmashauri makao makuu ambapo alisisitiza utendaji kazi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.