Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, Juma Sweda atoa Wito kwa Wawekezaji nchini kuwekeza Viwanda katika maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa lengo la kutoa ajira na kukuza uchumi wa Wilaya ya Misungwi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Wanahabari mapema jana katika ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama alipotembelea na kukagua Viwanda vya Sayona Steel LTD na Kiwanda cha Mkate cha Royal Supermaket vya Wilayani Misungwi, Juma Sweda amewataka wenye Viwanda kuendelea kuzalisha kwa wingi na kuwaomba Wananchi kutumia bidhaa zitokanazo na Viwanda vya ndani na hatimaye Soko la ndani litaendelea kuimarika zaidi.
Juma Sweda ametoa Wito kwa Wawekezaji na wenye Viwanda kuja kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambapo tayari wametenga Viwanja na eneo la Mitindo lenye Hekari 74 ambazo zinatolewa bure kwa Wawekezaji kwa ajili ya kujenga Viwanda vya kuzalisha bidhaa na vifaa vya aina mbalimbali na kuweza kutoa ajira kwa Wananchi wa Wilaya ya Misungwi.
Kwa upande wake Meneja Uzalishaji na Masoko wa Kiwanda cha Sayona Steel LTD cha Wilayani Misungwi, Sunny Naker amewaomba Wafanyabiashara na Wananchi wa Wilaya ya Misungwi na Watanzania wote kuvitumia bidhaa zinazozalishwa katika Kiwanda hicho zikiwemo masufuria,Steel wire na Nondo ambazo zinapatikana kwa wingi Kiwandani hapo.
Amesema kwamba biashara kwa muda sasa imesuasua kutokana na changamoto za mvua zilizokuwa zinanyesha na kusababisha kupungua kwa Wateja wa ndani na Soko la nje, na kueleza kwamba matarajio yao ni kuanza kuuza bidhaa za Nondo hivi karibuni baada ya Wananchi kuanza shughuli za ujenzi na kwamba wanatarajia kurejea katika uzalishaji wa Nondo na bidhaa zingine za ujenzi kama kawaida.
Katika ziara hiyo wameweza kukagua pia shughuli za ujenzi wa Kiwanda cha Mkate cha Royal Supermarket kinachojengwa maeneo ya Nyashishi Wilayani Misungwi ambapo ujenzi unaendelea vizuri na matarajio ya kukamilisha ni mapema mwezi Septemba mwaka huu baada ya kusimika mitambo ya uzalishaji wa bidhaa ya Mkate.
Mkuu wa Wialaya ya Misungwi, Juma Sweda (katikati) akiangalia Masufuria ambayo ni moja ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Sayona Steel LTD kilichopo maeneo ya Nyanghomango Wilayani Misungwi, (wa kwanza kulia ni Meneja Uzalishaji na Masoko wa Kiwanda hicho, Sunny Naker akifuatiwa baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya walioambatana na Mkuu wa Wilaya huyo katika ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda (kushoto) akikagua maeneo na kuona shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika Kiwanda cha Sayona Steel LTD kinachozalisha bidhaa ya Sufuria, Steel wire Nondo na bidhaa za zingine zinazotumika katika ujenzi,
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.