Mkuu wa Wilaya ya Misungwi akagua na kuridhishwa na Miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Misungwi na kuwataka wazazi kuwaruhusu wanafunzi wa kidato cha tano waliochaguliwa kuripoti kwa wakati kuendelea na masomo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha ametembelea na kukagua Shule ya Sekondari ya Misungwi Agosti,17,2023 ambapo ameridhishwa na Ujenzi wa bweni la wasichana ambalo limekamilika kwa asilimia 100 na lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 86 ambapo tayari wanafunzi 18 wamesharipoti shuleni ambayo ni sawa na asilimia 34.
Wakati wa ziara hiyo Mkuu Wilaya ya Misungwi Chacha amekemea vikali kwa wale watu wenye nia ovu ya kutaka kukwamisha ndoto za wanafunzi ikiwa pamoja na kuwapa mimba na kusisitiza hatawafumbia macho watu wa aina hiyo kwa kuchukuliwa hatua za kisheria na kutoa wito kwa wazazi na walezi kutoa ushirikano kwa wanafunzi na kuhakikisha wanafunzi wanatimiza malengo waliojiwekea.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Josefu Mafuru amesema kuwa wanahakikisha miundo mbinu na mazingira kwa ujumla yanakuwa salama na rafiki kwa wanafunzi ili kuleta utulivu na amani wakati wa kujifunza na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha kwa ujenzi madarasa pamoja na bweni la wasichana kidato cha tano na sita.
Naye Afisa Elimu wa Sekondari ya Wilaya ya Misungwi Bi.Diana Kuboja amesema jana wakati wa ziara hiyo ambapo amewahakikishia wanafunzi mazingira mazuri ya kujisomea pamoja na kupata chakula cha kutosha ili wapate wasaa mzuri wakati wa kujifunza kwa utulivu na umakini ili kupata matokeo mazuri katika mitihani yao.
Mwanafunzi Flova Davis wa kidato cha sita akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ameishukuru Serikali Kwa kuleta Walimu wa kutosha na kujenga madarasa mazuri na mabweni ambayo yanawavutia katika kujifunza na kuahidi kwamba watasoma kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika masomo yao ili kupata matokeo mazuri katika mitihani.
Mwonekano wa jengo la bweni la wasichana kidato cha tano na sita Shule ya Sekondari Misungwi ambalo limekamilika kwa asilimia 100 na lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 86.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.