Wahitimu wa Jeshi la Akiba waaswa kuchangamkia Ajira kwa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza,.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Veronica Kessy wakati akifunga mafunzo ya Jeshi la Akiba katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misungwi Mwanakanenge Wilayani humo mwishoni mwa wiki, na kuwataka kuchangamkia fursa kwa kuwa katika Vikundi mbalimbali kwa lengo la kujipatia kipato na kukuza uchumi wao binafsi, pia amewaasa wahitimu hao kuendelea kudumisha amani, utulivu na mshikamano uliopo na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo.
Akizungumza na Wananchi Bi. Veronika Kessy amewataka wahitimu hao kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kuwa waadilifu,kujituma na kuwa na moyo wa uzalendo katika kujenga nchi yao, sambamba na hilo amewataka kuanzisha vikundi na hasa vikundi vya afya na usafi wa mazingira na kuwa wajasiriamali wanaotambulika ili kuweza kujipatia mikopo ya Srikali kutoka Halmashauri itakayowawezesha kujikwamua na tatizo la ajira na kukuza uchumi wa familia zao..
Mkuu wa Wilaya huyo ameongeza kuwa Wananchi wa Misungwi kwa sasa wamehamasika na wanapaswa kuendelea kujitokeza kwenda kupata Chanjo ya UVIKO 19 ambapo Chanjo hiyo inasaidia kuongeza Kinga ya mwili na kupunguza makli ya ugonjwa pamoja na Vifo
Amewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya maambikizi ya Ugonjwa wa Corona na kuendelea kujikinga kwa kufuata na kuzingatia ushauri wa Wataalam wa Afya nchini kiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kuepuka misongamano, kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara pamoja na kufanya mazoezi.
Aidha, amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa hapo mwakani 2021,pindi muda utakapofika ili kurahisha zoezi hilo kwani lina manufaa makubwa kwa wananchi na hata kwa taifa kwa ujumla katika kupanga mipango yake ya maendeleo.
Kwa upande wake Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilayani Misungwi Meja Matemi amesema katika mafunzo hayo ambapo jumla ya Wahitimu 52 wamemaliza mafunzo hayo wakiwemo vijana wa kiume 39 na vijana wa kike 13, na kueleza na kuwataka Wahitimu hao kuwashukuru wazazi/walezi kuwaruhusu vijana wao kushiriki mafunzo na kuweza kuhitimu.
Wakati huo huo Meja Mateni amewataka wahitimu hao kuwa waadilifu na wazalendo katika kutumikia taifa lao kwa kujitoa katika shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja kuwa mstari wa mbele kusaidia taifa katika majanga na matatizo mengine yanapotokea.
Baadhi ya washiriki waliohitimu wamefarijika na mafunzo hayo na yamewajengea uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za kimaisha ambazo zinawakabili na zinazoweza kujitokeza katika shughuli zao za kila siku.
Mmoja wa Wahitimu wa Jeshi la Akiba, Bi. Prisca Augustine amewashauri vijana wenzake ambao bado hawajajiunga na Jeshi hilo kwamba wajiandae kufanya hivyo kwa manufaa yao wenyewe na taifa kwa ujumla kwani wanaweza kujipatia ajira kwa kuajiriwa katika makampuni mbalimbali pamoja na kujiajiri wao wenyewe kupitia fursa za vikundi vya ujasiriamali
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.