Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha ahimiza Wahe.Madiwani na Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa chakula katika Shule za Sekondari na Msingi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito ulitolewa mwishoni mwa wiki wakati wa Mkutano wa wadau wa Elimu uliofanyika katika ukumbi wa MGS Misungwi ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Paulo Chacha ambao ulilenga kujadili masuala ya uboreshaji wa Sekta ya Elimu sambamba na utoaji wa zawadi kwa shule za Msingi na Sekondari zilizofaya vizuri na zilizofanya vibaya pamoja na Walimu waliofanya vizuri katika Shule za Sekondari na Msingi.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha aliwataka Wahe,Madiwani,Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wa wanasimamia kikamilifu zoezi la kukusanya chakula cha kutosha katika maeneo ya Kaya za Wananchi hasa katika kipindi cha mavuno na kuhakikisha chakula kinapatikana cha kutosha mashuleni kwa ajili ya wanafunzi ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa Shule zote za Msingi na Sekondari.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Benson Mihayo alieleza kuwa mbali na Walimu hao kupewa zawadi fedha taslimu na vyeti pia Halmashauri imetoa viwanja kwa Watumishi hao kwa bei nafuu ambapo wanaweza kulipia kidogo kidogo na kupata kiwanja chenye ukubwa wa Mita za mraba 800 kwa thamani ya shilingi Milioni moja na laki sita kama motisha.
Kwa upande Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Bw.Martine Nkwabi aliekeza kwa Maafisa elimu Kata na Watendaji wa Kata na vijijini kuhakikisha wanasimamia kikamilifu na kuondoa utoro kwa wanafunzi kwa Shule zote za Msingi na Sekondari, wakati huo huo aliwataka kusimamia nidhamu mashuleni kwa Shule za msingi wahakikishe wanafunzi wanajua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Aidha, amesisitiza utoaji wa adhabu kwa wanafunzi uzingatie sheria na kanuni ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kwa mwanafunzi pamoja na kuzingatia ufundishaji mzuri unaozingatia lugha za ustaha, haiba kwa mwalimu na kuheshimu ratiba za masomo.
Afisa Ustawi Mwandamizi kutoka Mkoa wa Mwanza Bi.Rehema alieleza na kufafanua kuwa suala la uadilifu katika jamii nzima ni muhimu na nilazima kuzingatiwa ili kutengeneza kizazi bora cha sasa na kijacho ambapo aliwaomba Wadau mbalimbali wa elimu kutoa ushirikiano endapo wataona kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili kwa jamii zinazotunguka ikiwa ubakaji na ulawiti hasa kwa watoto.
Naye Afisa Elimu wa Sekondari Wilaya ya Misungwi Bi.Diana Kuboja alisema wataendelea kusimamia kikamilifu taaluma pamja na nidhamu mashuleni kwa Shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ili kukuza ufaulu na Kuondoa ziro kwa Shule zile ambazo zimefanya vibaya,na kwa kuwapa Walimu motisha chanya kwa wale wanaofanya vizuri na zoezi hilo litakuwa endelevu.
Mwalimu Diana Joseph ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Exodus Primary school ambayo ni shule binafsi ameishukuru Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa kutambua juhudi za walimu kwa kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu pamoja na vyeti na zoezi hilo limewapa hamasa katika kuinua na kuboresha kiwango cha elimu.
Kwaya ya Walimu wa Misungwi ikitumbuiza katika Mkutano wa Wadau wa Elimu katika ukumbi wa MGS wiki hii ambapo wadau mbalimbali walihudhuria Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Paulo Chacha akimkabidhi zawadi ya Cheti cha pongezi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Benson Mihayo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Elimu katika ukumbi wa MGS mapema wiki hii.
Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Bw.Martine Nkwabi kushoto akishuhudia Walimu wakikabidhiana kinyago kwa Shule iliyofanya vibaya katika matokeo ya Mitihani 2022.kama motisha hasi kwa Walimu hao.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.