Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi Bw, Petro Sabatto awataka Vijana wana kikundi cha Vijana kazi Kata ya Bulemeji kuvilinda na kuvitumia vizuri vyombo vya usafiri wa Pikipiki walizokepeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi zenye thamani ya shilingi milioni 26 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza..
Akizungumza katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika Hfla ya makabidhiano ya pikipiki Katibu Tawala Wilaya ya Msungwi Bw, Petro Sabatto kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Matiko Paul Chacha amesema Halmashauri zihakikishe zinanatenga fedha asilimia 10 kwa ajili ya kuwakopesha vikundi mbalimbali ikiwemo watu wenye ulemavu fedha hizo ambazo hutolewa na kurejeshwa bila riba.
Bw, Sabatto amesema na kuwaelekeza Vijana hao kuvilinda na kuvitumia vizuri vyombo vya usafiri wa Pikipiki kwa matumizi yaliyokusudiwa ili waweze kuwapa manufaa ya kiuchumi na kuinua kipato chao pamoja na kurejesha mikopo kwa wakati na kuruhusu wengine kukopa kwa ajili ya kunua uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
“Na Misungwi tunaenda vizuri na ninyi mkawe mabalozi wazuri kwa vijana wengine waweze kujiunga katika vikundi kupitia elimu inayoendelea kutolewa na Idara ya Maendeleo ya Jamii.” Alisisitiza Bw. Sabatto.
Akiwasilisha taarifa ya makabidhiano ya pikipiki hizo Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Misungwi, Bi.Juliana Mwongerezi amesema kuwa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 26 ambazo ni mkopo kutoka Halmashauri ambao umetolewa kupitia asilimia 4 ya fedha za mapato ya ndani kwa robo ya pili kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba 2022.
Aidha Bi.Mwogerezi ameongeza kuwa mbali na kukundi cha Vijana kazi kupata Mkopo isiokuwa na riba pia kuna vikundi vingine 5 ambavyo vimenufaika na mikopo hiyo kupitia fedha za mapato ya ndani kwa robo ya pili.Vikundi hivyo ni Mama Samia toka Kata ya Bulemeji kimepata mkopo wa shilingi milioni 8,000,000/= Amanina toka toka Kata ya Idedetemya shilingi Milioni 12,000,000/=,Wanawake Songambele toka Kata ya Mondo milioni 10,000,000/= na kikundi cha Mwamko toka Kata ya Idedetemya kimepatia shilingi Milioni 15,000,000/=na kufanya Jumla ya shilingi Milioni 56,365,000/ =ambazo zimekopeshwa mpaka hivi sasa.
Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi,Bw.Kashinje Machibya amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitekeleza Miradi mbali mbali ya maendeleo na kuwajali Wananchi wake kwa kuwapatia mikopo ambayo inatolewa na Halmashauri isiyokuwa na riba na bila kubagua Vyama vya Siasa hapa nchini.
Sambamba na hilo amewataka Kikundi cha Vijana Kazi kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili kurejesha mikopo hiyo kwa wakati na kuruhusu watu wengine kukopa fedha hizo, pia ametaka kuwa na mawazo makubwa ya kukopa fedha zaidi na kuwekeza katika miradi mikubwa yenye tija na maufaa zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Dkt, Chrispine Shami ameeleza kuwa ni kawaida kila robo ya mwaka wa fedha Halmashauri kutoa mikopo sawa sawa na utaratibu ambao zimewekwa na Serikali na kutoa wito kwa jamii nzima kupewa elimu juu ya mikopo inayotolewa na Halmashauri isiyokuwa na riba ili waweze kunufaika na mikopo hiyo kwa kufuata masharti,kanuni na taratibu ambazo zimeweka ili waweze kupata mikopo na kurejesha kwa wakati.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana kazi cha Kata ya Bulemeji Bw, Dotto Kaji Sylivester ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia mikopo ya pikipiki kupitia Halmashauri ambayo itawasaidia kuwanyanyua kiuchumi kwa kupitia pikipiki hizo ambazo wamekabidhiwa hivi mapema wiki hii, na kuahidi kulipa mikopo huo kwa wakati.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw.Petro Sabato(aliyevaa suti ya kijivu) akimkabidhi kadi ya Pikipiki mwenyeki wa kikundi cha Vijana Kazi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi,ambapo pikipiki hizo zina thamani ya shilingi Milioni 26 mapema wikii hii.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe, Kashinje Machibya,akiwaasa kikundi cha Vijana kazi kuzitumia pikipiki walizopewa kwa manufaa ili kujipatia kipato na kuweza kurejesha mkopo huo kwa wakati ambapo zoezi hilo lilifanyika katika maeneo ya ofisi za Halmashauri siku ya Jumatatu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Dkt, Chrispine Shami aliyesimama akitoa pongezi kwa kikundi cha Vijana kazi wakati wa makabidhiano ya Pikipiki siku Jumatatu ambapo vijana hao walikabidhiwa pikipiki 10 zenye thamani ya shilingi milioni 26.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi.Juliana Mwongerezi akitoa taarifa fupi ya Mradi wa usafirishaji abiria tarehe 30/01/2023 unaotekelezwa na kikundi cha vijana Kazi kata ya Bulemeji,ambapo Kikundi hicho kimekabidhiwa pikipiki 10 zenye thamani ya shilingi milioni 26 ni mkopo kutoka Halmashauri usiokuwa na riba.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana Kazi Bw.Dotto Sylivester akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya vijana wenzake katika ofisi za Halmashauri siku ya Jumatatu,amabapo walipokea pikipiki 10 zenye thamani ya shilingi Milioni 26 kupitia mkopo wa Halmashauri wa bila riba.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.