Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungw Bw. Abdiel Makangei awapongeza watendaji kwa kushirikiana na Madiwani kuongeza kasi na ufanisi katika ukusanyaji wa Mapato Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Wito huo umetolewa tarehe 29 Aprili 2025 katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo Bw. Makange amewataka watendaji pamoja na waheshimiwa Madiwani kushirikiana kwa pamoja kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Bw. Makange ameipongeza idara ya ya frdha na mapato ya Halmashauri na amesisitiza kuendelea na uwekaji mzuri wa mikakati ya bajeti na ukusanyaji wa mapato ili huduma za maendeleo ziwafikie wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe.Kashinje Machibya kupitia Baraza la Madiwani amemtaka Mkurugenzi kuendelea kusimamia kikamilifu mapato na matumizi ya fedha za Halmashauri pamoja menejimenti kwa ujumla wake, na kutoa rai kwa taasisi za Serikali kuendelea kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Wananchi.
Hata hivyo Bw. Machibwa ametoa rai kwa meneja wa TARURA kuhakikisha anatekeleza chabgamoto za Barabara katika maeneo mbalimbali yenye uhatibifu ikiwemo barabara za vijivijini kuingia mijini zinafanyiwa urekebishaji ili wananchi waweze kuondokana na adha hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama amesema kwamba ataendelea kusimamia kikamilifu Mapato ya Halmashauri kwa uadilifu mkubwa ili kufikia malengo ambayo Halmashauri imekasmia.
Kwa upande wao Wajumbe wa Baraza hilo walipongeza jitihada ya ukusanyaji wa mapato na kutoa mapendekezo mbalimbali ya kuboresha usimamizi wa miradi ikiwemo Barabara na kusisitiza umuhimu wa Miondombinu hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mkutano huo wa Baraza la madiwani ulihudhuriwa na Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Wataalamu kutoka katika Idara na Vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Misungwi pamoja na Wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.