Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Abdi Makange amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha anawashughulikia baadhi ya Watendaji wa Vijiji na Kata wasiokaa katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mhe. Makange ameyasema hayo leo Juni 28, 2024 katika Hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi amabapo amesema kwamba zoezi la Ukusanyaji wa mapato limekuwa na changamoto kubwa mojawapo ya sababu ni pamoja na kuwepo kwa asilimia 90 ya Watendaji wa Vijiji na Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi hawakai katika maeneo yao ya kazi hali hiyo inakwamisha utekelezaji mzuri wa Ukusanyaji wa mapato na kuelekeza suala hilo litatuliwe mapema iwezekanavyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama amemshukuru aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Joseph Mafuru hapo awali pamoja na uongozi wa Wilaya kwa ujumla kwa ushirikiano na maelekezo yote aliyopewa leo wakati akikabidhiwa ofisi kwa ajili ya kuanza majukumu na kuwaomba kuendelea kumpa ushirikiano pindi watakapohitajika.
“Napenda kuushukuru sana uongozi wa Wilaya ya Misungwi kama nilivyokusikia Mheshimiwa Katibu Tawala tayari umeanza kunipatia maelekezo na njia za kupita nashukuru sana kwa hilo na nitaendelea kufanyia kazi zaidi naomba ushirikiano kutoka kwa wenzangu na kwako pia” alieleza Mkurugenzi Mtendaji Addo Missama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe. Kashinje Machibya amewataka watumishi wa Halmashauri kuendelea kuongeza juhudi katika utendaji kazi na mabadiliko yaliyofanyika katika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yasiwe kikwazo katika uwajibikaji wao na badala yake wachape kazi na kutekeleza miradi na kuongeza mapato kikamilifu..
Mhe. Machibya amesisitiza kwamba anategemea Menejimenti kuongeza juhudi na kuendelea kumushauri Mkurugenzi Mtendaji na kumpa ushirikiano katika majukumu yake kadri watakavyo hitajika ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu na kuhakikisha Halmashauri ya Misungwi inasonga mbele kwenye sekta zote na kuwaletea Wananchi maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Addo Missama wa kwanza kushoto akisaini baadhi ya nyaraka wakati wa makabadhiano na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru leo tarehe 28,Juni 2024 katika ukumbi wa Halmashauri.
Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na baadhi ya Watumishi wa Makao Makuu Halmashauri wakifuatilia na kushuhudia makabidhiano hayo yaliyo fanyika leo 28,Juni,2024 katika ukumbi wa Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.