Billioni 2.8 zimetumika kutekeleza Miradi ya mpango wa TASAF hadi kufikia mwezi Machi 2017/2018,kwa lengo la kunusuru Wananchi katika Kaya 8641 za Wilaya ya Misungwi ambazo zinanufaika na mpango wa TASAF III .
Mjumbe wa Baraza la Madiwani,Mhe,Faustine Msafiri aliyesimama akichangia hoja katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa MGS
Akiwasilisha taarifa katika Baraza la Madiwani la robo ya tatu lililofanyika katika Ukumbi wa MGS ,Mhe Khalid Mbitiyaza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Kiuchumi,Mhe Mwamba Makune alieleza kwamba katika kipindi cha robo ya tatu mwezi Machi Halmashauri imeweza kutekeleza miradi 9 yenye fedha shillingi Billioni 2.8 katika mpango wa TASAF kwa kutoa ruzuku ya msingi na masharti pamoja na ruzuku kupitia ajira za muda kwa Walengwa ikiwa ni kuinua kipato na kuboresha maisha ya wananchi wa Wilaya ya Misungwi.
Akizungumza katika baraza hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Eliurd Mwaiteleke alisema Miradi imetekelezwa kwa kuzingatia kanuni ,taratibu na sheria za fedha na manunuzi yamefanyika kwa kufuata taratibu na miradi yote imetekelezwa kwa kiwango na ubora na Menejimenti inaendelea kutekeleza miradi kulingana na mapokezi ya fedha yanavyofanyika ili kuweza kufikia malengo kulingana na mpango na bajeti iliyopangwa.ambapo Halmashauri imeweza kupokea shillingi 3,187,088,669.05 na imetumia kiasi cha shillingi 2,872,463,179.kwa kipindi cha kuishia mwezi machi 2018 ambayo ni sawa na asilimia 90 ya fedha zilizopokelewa.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia mjadala na hoja mbalimbali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la robo ya tatu Januari hadi Machi 2018.
Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine baraza liliweza kupitia na kujadili miradi mbalimbali ikiwemo ya Sekta ya Afya, Maji ,Miundombinu ya barabara, Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari, Kilimo na Umwagiliaji, Utawala na Mifugo na Uvuvi ambazo zimetekeleza kikamilifu miradi ilipatiwa fedha kwa kipindi hicho na kukamilisha kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.