Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi lajadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi Bilioni 53.6 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza wakati wa kikao maalum cha Baraza la Wafanyakazi kwa ajili kutoa mapendekezo ya bajeti katika ukumbi wa Halmashauri, Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi Bw. Addo Missama ameeleza kwamba ni halali kwa kila mfanyakazi kutimiza wajibu wake na kusisitiza ushirikiano ili kuhakikisha wanafikia adhima na malengo yaliyowekwa na kuwaomba Watumishi waendelee kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Bajeti iliyopitishwa .
Bw. Missama ameongeza kuwa kikao hicho ni maalum kwa ajili ya kupitia na kufanya tathmini ya utendaji kazi ambapo kila mfanyakazi ana haki katika utekelezaji wa majukumu na stahiki anapowajibika kutimiza malengo yaliyopangwa hivyo amewasihi kufanya kazi kwa bidii na kwamba hakuna haki bila wajibu na kila mmoja tuendelee kufanya kazi kwa mujibu wa sharia , taratibu na miongozo.
Awali akiwasilisha rasimu ya Bajeti ya mwaka 2025/2026 Afisa Mipango wa Halmashauri Bi. Peniel Titus kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi amefafanua kwamba katika rasimu hiyo ya Bajeti kiasi cha shilingi 4,641,245,829/= ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha shilingi. Bilioni 41,888,608,000/= ni fedha ya mishahara ya Watumishi, na kiasi cha shilingi Bilioni 1,359,841,000/= ikiwa ni ruzuku ya uendeshaji ( OC) na kiasi cha shilingi Bilioni 5,725,139,282/= ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na fedha zote ni kutoka Serikali kuu.
Bi. Peniel Titus ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa rasimu ya bajeti hiyo ofisi ya Mipango na Uratibu imeahidi kutekeleza na kufanyia kazi mapendekezo na maadhimio ya kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha kuwa na maendeleo chanya katika jamii ndani ya Halmashauri ya Misungwi.
Kwa upande Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Mwanza Bw. Aloysius Mapembe amesema mapendekezo ya Bajeti hii ya mwaka wa fedha 2025/2026 yamendaliwa na kuwasilishwa kwa weledi na umakini na kupongeza uwasilishwaji wake ambapo pia amempongeza Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Misungwi kwa kuwa na timu yenye kujituma na kuandaa vyema taarifa ya Bajeti pamoja na kikao hicho.
Baraza hilo la Wafanyakazi limehudhuriwa na wajumbe ambao ni Wawakilishi wa Watumishi wa kila Idara na Vitengo, Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri ya Misungwi, Viongozi wawakilishi wa Vyama vya Wafanyakazi kwenye ngazi ya matawi, ngazi ya Wilaya pamoja na Viongozi wa ngazi ya Mkoa.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.