Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi laridhia na kupitisha Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi Bilioni 51.5 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza jana tarehe 1 Februari 2024 wakati wa kikao maalum cha Baraza hilo katika ukumbi wa Halmashauri ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya amesema rasimu hiyo ya Bajeti ya kiasi cha shilingi. Bilioni 51.5 itasaidia kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa pamoja na kuongeza na kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii kama vile huduma za Sekta ya Elimu, huduma za Afya, maendeleo ya jamii , mazingira, ambapo katika rasimu hiyo kiasi cha shilingi. Bilioni 8.6 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za miradi maendeleo.
Mhe, Machibya ameeleza kwamba Baraza la Madiwani halitokuwa tayari kumvumilia Kiongozi ama mfanyabiashara yoyote atakayesababisha na kuleta ukwamishaji katika suala la Ukusanyaji wa Mapato kwa kuzingatia kuwa kipaumbele cha Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ni Mapato, Mapato Mapato kwa mfulululizo kwa lengo kuu la kuwaletea maendeleo Wananchi wa Wilaya hiyo.
Mhe, Machibya amesema kwamba Baraza la Madiwani lina wajibu wa kusimamia mapato ya ndani kwa bidii kwa maslahi mapana ya Wananchi na kuhakikisha kutokutoa mwanya wa upotevu wa mapato kwa namna yeyote ile na kuwataka Watendaji wa Kata kuendelea kusimamia na kutumia kikamilifu fedha za Miradi ya Maendeleo katika Kata zao vizuri na ziendane thamani ya fedha katika miradi hiyo wanayoisimamia.
Awali akiwasilisha rasimu ya Bajeti ya mwaka 2024/2025 Afisa Mipango Bi. Peniel Titus kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi amefafanua kwamba katiaka rasimu hiyo ya Bajeti kiasi cha Bilioni 4.7 ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha shilingi. Bilioni 36.7 ni fedha ya mishahara ya Watumishi,kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 ni ruzuku ya uendeshaji ( OC) na kiasi cha Bilioni 8.6 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na fedha zote ni kutoka Serikali kuu.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi Bw. Leonidas Kondela ameipongeza Halmashauri kwa kubuni na kupanga kuanzisha ujenzi wa Shule ya awali na Msingi itakayowezesha watoto wa Wilaya ya Misungwi kupata elimu bora na ya uhakika pia amewaomba kwa msisitizo Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wataalam wote kuhakikisha wanasimamia fedha za Miradi ya maendeleo kwa umakini mkubwa ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw.Joseph Mafuru amesema Bajeti hii ya mwaka wa fedha 2024/2025 ni lazima itekelezwe kwa kuchukua hatua madhubuti katika ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na fedha zinazotoka Serikali kuu kwa ajili Miradi mbalimbali ya maendeleo zitasimamiwa vizuri kwa maslahi mapana ya Wananchi ambapo shilingi. Milioni 300 kutoka mapato ya ndani zitaweza kutekeleza ujenzi wa shule ya awali na msingi na kuwanufaisha watoto wa Wilaya ya Misungwi na kuwa chanzo kimojawapo cha mapato ya ndani yenye uhakika.
Wakati huo huo,Diwani wa Viti Maalum Dotto Sembelu amesema Bajeti ya kiasi cha shilingi. Bilioni 51.5 ambapo kati hizo kiasi cha shilingi Bilioni 4.7 ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri, ameeleza kuwa Madiwani na Watendaji wanawajibu wa kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhakikisha fedha hizo zinapatikana na kwenda kufanya shughuli za maendeleo kwa wananchi pia amemshukuru Mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo fedha za ujenzi wa madarasa na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari wa ajili utekeleza wa Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waheshimiwa Madiwani wakijadili na kupitisha Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi tarehe 01/20/2024.
Wakuu wa Taasisi,Idara na Vitengo wakisikiliza na kujadili Bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 mapema jana katika ukumbi wa Halmashauri ambapo Bazara limepitisha Bajeti ya shilingi Bilioni 51.5
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.