Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Misungwi lapitisha rasmi ya Bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yenye jumla ya shilingi Bilioni 54.6 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza jana mapema wakati wa kikao maalum cha Baraza hilo katika ukumbi wa Halmashauri ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya amesema rasimu hiyo ya Bajeti ya kiasi cha Bilioni 54.6 , Bilioni 4.8 ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha Bilioni 40.6 ni ruzuku ya mishahara,kiasi cha Bilioni 1.02 ni ruzuku ya uendeshaji, itasaidia kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa pamoja na kuongeza na kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii kama vile umeme maji na huduma za Afya,ambapo katika rasimu hiyo kiasi cha Bilioni 7.7 kimetengwa kwa ajili ya fedha za miradi maendeleo.
Mhe, Machibya amesema kwamba Baraza la Madiwani lina wajibu wa kusimamia mapato kwa bidii kwa maslahi mapana ya wananchi na kuhakikisha kutokutoa mwanya wa upotevu wa mapato kwa namna yeyote ile na kuwataka watendaji wa Kata kuendelea kusimamia na kutumia kikamilifu fedha za Miradi ya Maendeleo katika Kata zao vizuri na ziendane thamani ya fedha katika miradi hiyo wanayoisimamia.
Awali akiwasilisha rasimu hiyo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bi.Mwanajumbe Zuberi ambaye ni Afisa Mipango ameeleza katika rasimu hiyo ya Bajeti kiasi cha Bilioni 54.6, Bilioni 4.8 ni fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri ,kiasi cha Bilioni 40.6 ni ruzuku ya mishahara,kiasi cha Bilioni 1.02 ni ruzuku ya uendeshaji ( OC) na kiasi cha Bilioni 7.7 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na fedha hizo ni kutoka Serikali kuu.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw.Petro Sabato kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, amesisitiza kwa Waheshimiwa Madiwani, Taasisi mbalimbali za Serikali na Viongozi na Wataalam wote kuhakikisha wanasimamia fedha za Miradi ya maendeleo kwa umakini mkubwa ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Bw.Benson Mihayo amesema rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 ni lazima itekelezwe kwa kuchukua hatua madhubuti katika ukusanyaji wa mapato ya ndani lakini pamoja na fedha zinazotoka Serikali kuu kwa ajili Miradi mbalimbali ya maendeleo zisimamiwe vizuri kwa maslahi mapana ya Wananchi.
Diwani wa Kata Mbarika na Mwenyekiti wa Kamati Huduma za Jamii Mhe,Joel Dogani amesema Bajeti ya kiasi cha Bilioni 54.6 ambapo kati hizo kiasi cha Bilioni 4.8 ni mapato ya ndani ya Halmashauri, ameeleza kuwa wanawajibu wa kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhakikisha fedha hizo zinapatikana na kwenda kufanya shughuli za maendeleo kwa wananchi pia amemshukuru Mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo fedha za UVIKO kwa ajili utekeleza wa Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali na Washeshimiwa Madiwani wakiendelea kujadili na kupitisha Bajeti yenye jumla ya kiasi cha Bilioni 54.6 ya mwaka kwa fedha 2023/2024 katika ukumbi wa Halmashauri hapo jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya misungwi Mhe,Kashinje Machibya aliyesimama akiongoza mkutano wa Baraza wakati wa kupitisha bajeti yenye kiasi cha Bilioni 54.6 ya mwaka kwa fedha 2023/2024 katika Ukumbi wa Halmashauri siku ya Jumanne tarehe 21/02/2023
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.