Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, limepokea na kuridhia matumizi ya Tshs. 1,432,582,811 zilizotekeleza shughuli na Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika kipindi cha robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba kwa mwaka 2017/2018 .
Akitoa taarifa ya Miradi iliyotekelezwa kwa robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba 2017 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbai MGS Hotel Misungwi Mwenyekiti wa Halmashauri,Mhe, Antony Bahebe Masele alisema kwamba, Halmashauri ya Wilaya ilipokea kiasi cha Tshs. 420,052,052 sawa na asilimia 4.66% ya fedha zilizopangwa kwa Mwaka Mzima ambazo ni Tshs. 9,021,332,000. za kutekeleza MIradi ya Maendeleo, Vile vile Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 1,087,969,521.37 toka TASAF za kutekeleza mpango wa kunusuru Kaya Maskini na kufanya jumla ya mapokezi yote kuwa Tshs. 1,508,022,041.37
Mhe,Masele alieleza kuwa na kutumia kiasi cha Tshs. 1,432,582,811 sawa na asilimia 95% ya fedha zilizotolewa kutekeleza Miradi mbalimbali kwa kipindi hicho ikiwemo Miradi ya Sekta ya Utawala,Elimu Msingi,Mifugo, Mipango,TASAF na Mfuko wa Jimbo ambapo Miradi yote imetekelezwa kwa kiwango na ubora na kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Utekelezaji Miradi kwa robo ya kwanza ilieleza na kuonyesha kwamba katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2017/2018, Halmashauri ya wilaya imepanga kutumia kiasi cha Tshs. 9,021,332,000/= kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Sekta za Afya, Elimu, Maji, Ardhi, Ujenzi, Mipango, Maendeleo ya Jamii, Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Mifugo na Uvuvi, Mazingira na Utawala. Fedha hizo zitatoka katika Vyanzo Mbalimbali navyo ni Serikali Kuu, Halmashauri ya Wilaya, Busket Fund, NRWSSP, Mfuko wa Jimbo, SEDP, TASAF, TACAIDS, Road Fund, LGDG na Michango ya Jamii.
Aidha, taarifa hiyo pia ilionyesha kwa Muhtasari namna Mapokezi na Matumizi ya Fedha za Maendeleo kuishia 30, Septemba 2017 yalivyokuwa kwa kila Sekta kama ifuatavyo:
Na
|
Jina la Mradi
|
Fedha pangwa
|
Fedha tolewa
|
Fedha tumika
|
1 |
Miradi ya Mapato ya Ndani (60%)
|
1,237,427,000 |
42,492,432 |
42,492,432 |
2 |
Rural Water Supply and Sanitation
|
3,935,836,000 |
0 |
0 |
3 |
Health Sector Basket Fund (HSBF)
|
759,931,000 |
0 |
0 |
4 |
Local Govt. Capital Devt. Grant (LGCDG)
|
1,776,225,000 |
0 |
0 |
5 |
Mfuko wa Jimbo (CDCF)
|
67,917,000 |
33,956,000 |
0 |
6 |
Capitation Secondary
|
79,040,000 |
22,284,180 |
22,284,180 |
7 |
School Meals Secondary
|
50,537,000 |
11,714,592 |
11,714,592 |
8 |
Fidia ya Ada Shule za Kutwa Sec
|
180,680,000 |
40,367,939 |
40,367,939 |
9 |
Head Masters Allowance SEC
|
69,000,000 |
11,500,000 |
11,500,000 |
10 |
Capitation Prim School
|
351,225,000 |
124,281,565 |
124,281,565 |
11 |
Special School Prim School
|
101,314,000 |
30,405,812 |
30,405,812 |
12 |
Ward Educ. Coordinators Prim School
|
81,000,000 |
20,250,000 |
20,250,000 |
13 |
Head Teachers Allowance Prim School
|
331,200,000 |
82,800,000 |
82,800,000 |
14 |
TASAF
|
0 |
1,087,969,521.37 |
1,046,486,291 |
|
Jumla Kuu
|
9,021,332,000 |
1,508,022,041.37 |
1,432,582,811 |
Mhe, Bahebe Masele aliongeza pia kuhusu matumizi ya fedha za Bakaa ambapo Halmashauri ya Wilaya imeendelea kutekeleza Miradi ya bakaa ya Mwaka 2016/2017 yenye thamani ya Tshs. 129,118,748 na Matumizi yaliyofanyika kuishia Septemba kufikia Tshs. 71,445,429. ambazo zimetekeleza miradi ya Sekta mbalimbali kama inavyoonyesha hapa chini :
NA |
JINA LA MRADI |
FEDHA ILIYOKUWA IMEBAKI |
FEDHA TUMIKA |
1 |
HSBF
|
54,821,243 |
52,555,309 |
2 |
Maombi Maalum
|
60,979,385 |
5,572,000 |
3 |
Mfuko wa Jimbo
|
717,000 |
717,000 |
4 |
LGDG
|
11,704,120 |
11,704,120 |
5 |
AGPAHI
|
897,000 |
897,000 |
|
Jumla Kuu
|
129,118,748 |
71,445,429 |
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.