Baraza Madiwani la pongeza na kuridhishwa na juhudi za ukusanyaji wa Mapato ya ndani Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya ameyasema hayo jana wakati Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya nne 2022/2023 katika Ukumbi wa Halmashauri kuwa mwaka 2022/2023 Halmashauri ilikasmia kukusanya Bilioni 3.1 na mwaka 2021/2022 Bilioni 2.3 ambapo ongezeko Zaidi la asilimia 26 kwa malengo yaliyowekwa.
Aidha Bw,Machibya amesema kuwa waliweza kupeleka kwa mkupuo Zaidi ya fedha Milioni 270 kwenye Kata zote 27 kwa ajili ya ukamilishaji wa Miradi mbalimbali katika maeneo yaliyo pangwa. Lakini kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imeksamia kukusanya kiasi cha fedha Bilioni 4.8 na tayari Mwezi Julai wamesaanza kusanya mapato na kuanza utekeleza katika Mwaka mpya wa fedha.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Usimamizi,Ufuatiliaji na Ukaguzi Mkoa wa Mwanza Bw, Kusirie Swai ametoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi pamoja na ushrikiano wa Waheshimiwa Madiwani kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa Mapato ya ndani na kutoa rai kwa taasisi ya TARURA,TANESCO,RUWASA kuchukua hatua madhubuti za kuwatumikia Wananchi katika kutatua changamoto walizo nazo kwa wakati.
Diwani wa kata ya Mbarika Mhe,Joel Dogani amesema kuwa watasimamia na kuhakikisha wanakusanya Mapato kama agizo la Mhe,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba Halmashauri zote nchini zikusanye mapatoya kutosha ili kukidhi mahitaji ya Wananchi.
Sambamba na hilo amesisitiza kuwa kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri iliweza kupeleka fedha kiasi cha shilingi Milioni 10 kwa kata zote 27 kutoka kwenye makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya kwenda kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Naye Diwani wa viti maalumu Mhe, Adelina John ametoa shukrani zake za pekee kwa Madiwani kwa ushirikiano na mshikamano ambao wanautoa katika kuhakikisha wanasimamia vizuri makusanyo mapato ya ndani ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Katibu Tawala Msaidizi Usimamizi,Ufuatiliaji na Ukaguzi Mkoa wa Mwanza Bw, Kusirie Swai aliyesimama akitoa maelekezo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani hapo jana ambapo aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa mikakati mizuri ya ukusanyaji Mapato ya ndani.
Waheshimiwa Madiwani wakishiri kikao cha Mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya nne hapo jana katika ukumbi wa Halmashauri ambapo walifurahishwa na ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuwataka watendaji wenye dhamana kusimamia vizuri Miradi ya maendeleo.
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wakisikiliza kwa makini mjadala ukiendelea wakati wa Mkutano wa baraza la Madiwani jana katika ukumbi wa Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.