Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Misungwi laipongeza Menjimenti kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kuishia Juni mwaka 2021/2022 kwa asilimia 108 Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe, Kashinje Machibya alieleza kwamba Baraza la Madiwani limepongeza na kuridhika na juhudi na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo kwa mwezi kuanzia Februari hadi Agosti kwa siku wamekadiria kukusanya shilingi 8,800,000/= ambapo kwa Mwaka wamekasimia kupata shilingi Bilioni moja nukta moja kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Mhe, Machibya amesema kwamba kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri iliweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa Mapato ambapo iliweza kusanya shilingi Bilioni 2.5 ambapo wamevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa asilimia mia moja na nane na wamejipanga kwa dhati kuhakikisha wanatekeleze kwa vitendo ili kuongeza mapato ndani ya Halmashauri .
Akizungumza katika Baraza la Madiwani Mhe, Machibya amewashukuru sana washeshimiwa Madiwani,Mbunge,Wakuu wa Idara,Vitengo na wajumbe wote kwa ujumla wake kwa kuchangia hoja na kutoa ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha wanakuwa malengo ya pamoja kuweza kufikia yale waliyoyapanga katika usanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
“Kwa niaba yenu wote kwa ujumla nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassani na Mbunge ,kwa mwaka wa fedha 2021/2022 tumepokea shilingi bilioni 13.0.97 fedha za maendeleo kutoka Serikali Kuu na fedha za mapato ya ndani ni zaidi shilingi milioni mia sita na bakaa ambayo inaendelea kutumika na niwapongeze sana”.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi Bw. Benson Mihayo amesema kwamba Menejimenti itaendelea kukusanya mapato kwa bidii ili kufikia malengo waliojiwekea katika Halmashauri ili kuendelea kutatua changamoto za Wananchi kwa kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Bw. Benson Mihayo amesema kwamba Halmashauri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/ 2022 imeweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kutoka katika vyanzo vya ndani vya mapato sawa na asilimia 100.8 na kusisitiza kwamba Menejimenti wamejiwekea mikakati ya kuendelea kukusanya Mapato na zoezi linaendelea vizuri ambapo wajiwekea maksio ya shilingi milioni 8.8 kwa Mwezi na kwa mwaka wa fedha 2022/23 wamekadiria kukusanya shilingi bilioni 3.1.
Alifafanua kuwa fedha zinazoletwa na Serikali ni lazima zisimamiwe vizuri pamoja na miradi iliyopo ili iweze kuwaletea maendeleo Wananchi pasipo kuwa na upotevu wa fedha,na kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi ya fedha ambazo Serikali inaendelea kuzitoa ni kwa ajili maslahi ya Taifa.
Wakati huo huo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Misungwi Bw.Mohamed Ally Chorage alisisitiza Madiwani wahakikishe wanasimamia fedha zote za miradi kwenye maeneo yao ili ziweze kuleta maendeleo kwa wananchi aidha aliwataka Waheshimiwa Madiwani kuhakiksha wanatimiza majukumu yao na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa manufaa ya Wananchi kwa ujumla,
Pia alisisitiza kuwa Elimu na hamasa iendelee kutolewa kwa Wananchi kuhusiana zoezi la Kitaifa la Sensa kuondoa dhana potofu kwa baadhi ya wananchi juu ya Sensa kuanzia ngazi za Vitongoji,Vijiji na Kata kwani kufanya hivyo itasaidia kufanikisha watu kuhesabiwa ,ambapo zeozi hilo linatarajiwa kufanyika siku ya kuamkia tarehe 23/Agosti/2022.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mbarika Mhe, Mhe Joel Dogani amesema hali ya Mapato kwa sasa iko vizuri ambapo wanakusanya wastani shilingi 16,000,0 00/= kwa siku.Sambamba na hilo ameahidi watasimamia kwa vitendo na wamejipanga kimkakati katika ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 watahakikisha wanafikia malengo ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.1ambapo malengo hayo yanawezekana kutimia endapo watashikana kwa pamoja ili kufkia malengo hayo waliojiwekea.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia mjadala kwa umakini katika mkutano wa Baraza la Madiwani katka ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe,Kashinje Machibya akiongoza mjadala wa Madiwani katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi,na kuwapongeza pamoja na Timu Menejimenti kwa ujumla kwa kusimamia vizuri Ukusanyaji wa mapato.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.