Balozi wa Pamba nchini Mhe,Aggrey Mwanri aagiza Watendaji na Wataalamu kutoa Elimu kwa Wakulima kuhusu kilimo cha kisasa cha zao la Pamba Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Agizo limetolewa na Mhe,Aggrey Mwanri katika ziara ya kutembelea na kuelimisha Wananchi kwa siku nne katika Vijiji 11 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ambapo aliwataka Wataalamu wa Kilimo kuendelea kuelimisha Wakulima katika maeneo yao kwa kulima zao la pamba kitaalamu na kwa tija ili kuzalisha mazao mengi katika eneo dogo.
Mhe, Mwanri ametoa wito huo kwa Maafisa Kilimo na Watendaji wa Kata kuendelea kutoa mafunzo kwa Wananchi juu ya kilimo cha kisasa cha zao la pamba kwa kutumia mbegu bora na namna sahihi ya matumizi ya viuatilifu na kufuata maelekezo ya wataalamu watakayopatiwa katika mafunzo ili kuongeza pato kwa ngazi ya kaya na Halmashauri kwa ujumla.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Abdi Makange kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe,Paulo Chacha amesistiza nidhamu kwa watumishi wa umma kuwa na nidhamu ya kazi ili kuwatumikia Wananchi kikamilifu kuheshimiana na kushirikiana kwa pamoja na hatosita kumchukulia hatua mtumishi yoyote atakaye kwenda kinyume na maagizo alioyatoa ,pia ameagiza kila mwananchi alime heka moja ya zao la pamba ili kufikia malengo yalio kusudiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Christopher Legonda ameelekeza kwa watendaji wote ngazi ya kata na vijiji kuhakikisha wanahamasisha wananchi kujiandaa na kilimo katika maeneo yao ili kuendana na msimu wa mvua kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.
Kwa upande mwingine Bw.Legonda amesema kuwa zoezi la dirisha la uandikishaji kwa watoto wanaotakiwa kujiunga na elimu ya Awali na darasa la kwanza lifanyike mapema kabla ya tarehe 30 Disemba Mwaka huu na maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza .
Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Misungwi Bi, Esther Mcharo amesema kuwa wakulima wanatakiwa kufuata ushauri wa wataalamu namna ya kulima kisasa zao la pamba ili kuleta tija na kupata mazao mengi ambapo amewataka wakulima kufuata kanuni kumi za namna ya kulima zao la pamba ikiwa ni pamoja na kutayarisha shamba mapema kutumia mbolea za samadi ,kupanda pamba mapema,kupanda kwa mstari na kwa idadi halisi ya mbegu katika kila shimo na kupalilia kwa wakati ili kuvuna pamba na kuichambua mapema huku unyunyuziaji wa dawa ukizingatiwa wakati wa ulimaji huo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kanyelele Bw,Thomas Ishunasho ametoa shukrani za pekee kwa ujio wa Balozi wa pamba hapa nchini kwa kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha zao la pamba kwa Wilaya ya Misungwi ambapo kwa kupitia mafunzo hayo wameweza kupata elimu ya kutosha na kuahidi kwenda kuwaelimisha wananchi namna nzuri ya kulima zao la pamba katika kata zao.
Balozi wa Pamba nchini Bw,Aggrey Mwanri akielekeza na namna ya unyunyuziaji wa dawa katika zao la pamba wa kufuata mistari ya halisi ya eneo la shamba.
Wataalamu wa Kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakionyesha namna ya uchimbaji wa mashimo wakati kupamba mbegu bora za zao la pamba.
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Ufagaji na Uvuvi Dr Crispine Shami akisoma taarifa fupi ya ziara katika Ukumbi wa Halmashauri leo mapema ambapo alitoa shukrani kwa kufanyika Mafunzo ya namna ya kulima kisasa zao la pamba katilka Wilaya ya Misungwi.
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.